Friday, May 29, 2009

JE MWENZANGU NI LINI MARA YA MWISHO UMEKULA MUWA?


Hapo kazi na mtu nipo katika shamba langu la miwa, nakata miwa kuwahi sokoni.

13 comments:

  1. Yasinta na wewe na maswali yako!!! ngoja nifikirie halafu ntakujibu

    ReplyDelete
  2. Mimi napinga, mkataji miwa kwenye picha hiyo, asilani si wewe!!

    ReplyDelete
  3. Dada Mariam fanya haraka!

    Chib kwa nini unafikiri si mimi. Vp tayari upo Bongo au?

    ReplyDelete
  4. Piga ua galagaza, mkata miwa siyo wewe.
    Miwa?
    Mi mara ya mwisho nimekula saa 6 mchana huu.
    Najua we huli miwa huko uliko. Usibishe!
    Ni hayo tu!

    ReplyDelete
  5. umenikumbusha miaka ya nyuma sana tulienda safari ya kimasomo mikumi , kidatu na Kilombero kwenye mashamba ya miwa, basi Mashambani tuliingia asubuhi wakati hatujanywa hata chai na tukaruhusiwa kula miwa tani yetu ila tusibebe, we ilikuwa balaa tulikula weeee lakini mwisho tulibeba pia si unajua wanafunzi tena, ah ngoja nikanunue vipande vya miwa barabarani maana mmenitamanisha

    ReplyDelete
  6. uongo mbaya mara ya mwisho sikumbuki ila nilipokuwa shule ya msingi tulikuwa tunakula sana na wenzangu break time tunaenda sokoni kununua miwa kila mmoja na kipande chake tunamenya na mdomo tunakula kwani shule yetu pale mwanza ilikuwa inatizamana na soko kuu, lakini mwaka jana nilipoenda dar xmas, nikauliza hivi wale jamaa wanao uza miwa barabarani kwenye madaladala hawapo, wakanijibu subiri hatujafika sehemu walipo, mara tukafika sehemu walipo, wakaniuliza je umewaona sasa tukununulie nikakataa kwani nilikuwa nataka kuwaona tu, kwani ile style yao ya kupuliza mifuko halafu wanaweka miwa nilikuwa siipendi ila nilikuwa nakunywa sana juice ya miwa pale kisutu karibu na maduka ya jumla wakati nafanya kazi dar sijui mpaka leo kama bado ipo, hivyo nipe tena muda nifikirie zaidi

    May 29, 2009 4:25 PM

    ReplyDelete
  7. Hapa nilipo nina kipande cha muwa,
    si utamu huo!!!!!!

    ReplyDelete
  8. Je una maana ya aina ipi ya muwa? kuna miwa ya aina mbali mbali..fafanua tafadhali!!

    ReplyDelete
  9. mmumyhery utaki jamaa wapulize? kwani hujuwahi kuutafuna muwa wa mtu mdomo......

    mimi natafuna saaana miwa bongo hii. sio kwenye dala dala wala njiani kwani napendelea kutembea kwa miguu kama zaoba vile

    ila sijui unamaanisha muwa upi maanake lazima ufanye zszshhhhhiii ili kufyonza utamu, maji

    ReplyDelete
  10. Miaka kumi iliyopita,Forodhani Zanzibar, duh! Yasinta wewe na uchokozi wako!haya bwana endelea kutukumbusha na kututamanisha.

    ReplyDelete
  11. Kamala swali lako gumu kidogo sijalielewa vizuri, Yasinta sasa kuokoa muda wa kufikiri nimemuagiza rafiki yangu mthailand, yeye akiagiza kwao leo kesho utafika ukifika nikisha kula natakufahamisha.

    ReplyDelete
  12. nhe hehe, ati unakata miwa kuwahi sokoni? unawahi sokoni wakati muda unaokata miwa tayari ni mchana kweupe pe? ulilala hadi saa nne ndiyo ukate miwa kisha uwahi sokoni? Umeshachelewa. Hiyo miwa iweke pale chini ya mti, ifunike vizuri na majani ya ng'ombe au gunia, siku ya gulio ikifika udamke alfajiri yake uiwahishe.
    Mara ya mwisho nimekula miwa Agosti 2008.
    Mara ya mwisho nimenunua juisi ya miwa ya kopo nikaichanganya mwenyewe na ndimu na tangawizi, hiyo ilikuwa mwezi wa Aprili 2009.
    Nimekumbuka wakati mmoja nikiwa mdogo na mroho wa miwa nilikuwa namenya maganda habati mbaya limenikata kiganjani, bibi akaenda ndani akachukua kikopo chake chenye dawa ya rangi ya kahawia, kali hiyo, anasema nakupa 'tinch', lete mkono upate 'iodine'.
    Halafu kila nilipokuwa nakazana kumenya mua, lazima unichune mdomoni halafu nikila chakula chenye chumvi jioni ndiyo nasikia habari ya maumivu yake.
    Maisha historia!

    ReplyDelete
  13. Nyumbani kuna miwa mingi utadhani mashamba ya miwa ya Mtibwa au kilombero. Cha ajabu mwezi unaweza kuisha bila kula hata kipande kimoja.

    ReplyDelete