Leo nimeona nijikumbushe kidogo maneno ya kiswahili kisije kikaniacha. Kama si sahihi naomba msaada:-
Muungwana = Mtu mwenye adabu na desturi njema, mtu anayekaa na binadamu wenzie kwa uzuri, mtu mwenye utu. Pia unaweza kusema mtu asiye mtumwa au jina la heshima analoitwa mtu.
Mvumilivu = Mtu anayestahamili taabu au mambo mazito (mstahamilivu).
Ngangari = Mtu mwenye msimamo.
Fadhila = Wema, ukarimu, hisani, huruma.
Wema = Ni hali ya matendo mazuri.
Ukarimu= Utoaji vitu au mali kwa kukaribisha watu au kuwasaidia wanaohitaji msaada bila ya malipo. Ni kinyume cha ubahili.
Hisani = Moyo wa kutaka kutenda mazuri kwa ajili ya mwingine.
Huruma = Moyo wa wema; imani, rehema na upole.
1. Imani ni mambo anayokubali mtu kuwa ni ya kweli na anayopaswa kuheshimu hasa katika dini: itikadi. Na pia ni maoni ya moyo yanayomfanya mtu awe na mkabala fulani juu ya jambo au kitu.
2. Rehema ni neema anazopata binadamu kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Na neema ni hali ya kuweko na uwingi wa nafasi; hali ya kutoweko shida au upungufu wa vitu vya kumuendeshea binadamu maisha; baraka na ustawi. Pia ni jambo jema analopata kiumbe kutokana na uwezo wa Mwenyezi Mungu; riziki.
3. Upole ni hali ya kutopenda fujo, hali ya mtu mtulivu na mtaratibu.
Thamini = Gharama au ubora wa kitu kutokana na hali na kuhitajika kwake na jamii.
Na mwisho ni, Si bitozi = Asiyejisikia.
Hongera sana kwa kuithamini lugha yetu adhimu.
ReplyDeleteNgangari!!! Umenikumbusha mambo ya CUF.
ReplyDeleteKesho naenda nyumbani Tanzania. Nina hamu sana ya kuzungumza kiswahili kwa uhuru mahali popote
Asante Fadhy! KiSwahili ni lugha yangu na sitaki kusahau na sitasahau na ninajivuna sana kwa hili.
ReplyDeleteChib! nawe asante kwa kuwa mkfuatiliaji mzuri wa blog yangu. Nakuonea WIVU kwenda nyumbani na kuongea kiswahili kwa uhuru na popote kama usemavyo. Nachukua nafasi hii kukutakia SAFARI NJEMA.
Nimefurahia neno Muungwana, kuna hadithi ya michoro katika gazeti la sani jamaa anaitwa MUUNGWANA alikuwa mng'arisha viatu akapata mali ghafla kutokana na uungwana wake wa kumsaidia mtu maisha yake yakabadilika ghafla
ReplyDeleteChib unakuja bongo tuwasiliane mkuu sio vibaya kama utakuwa dsm
Asante kwa hili!
ReplyDeleteChib ,vipi lakini Kiswahili hapo Rwanda, haiwezekani kuishi kwa kutumia kiswahili pekee hapo?
vimax thanks gan infonya vimax asli di tunggu info selanjutnya gan obat klg
ReplyDelete