Nimepita ktk kibaraza cha kwa kaka Ramadhani msangi http://www.uchambuzi.blogspot.com/nimeona maswali haya ni maswali mazuri na ni kweli hata mimi nimekuwa nimejiuliza "hivi haya maswali hutokana na nini hasa?" je mtu huwezi kuongea tu bila kuuliza maswali? (Pia yamenigusa kwani binafsi ni mtu wa maswali sana:-)
Limekuwa ni jambo la kawaida sana ambalo limeshazoeleka, kuwa unapokutana na washkaji zako mitaani wanakuuliza kwanini hiki, mara kwanini kile nakadhalika.
Chukulia mfano ulikuwa unafanya kazi, unapoacha au kuachishwa kazi, watu watakuuliza kwanini umeacha au kuachishwa kazi? Kama ulikuwa na demu, mchumba, mke au rafiki na ukaachana naye, watakuuliza kwanini uliachana naye.
Kama ulikuwa unatembea kwa gari na siku ukaamua kuzurura mitaani kwa mguu watakuuliza mbona huna gari leo, na maswali mengine kama hayo. Ninachojiuliza ni kuwa mbona uulizaji wa maswali haya huzingatia upande mmoja zaidi?
Mbona unapokuwa kazini hakuna anayekuuliza kwanini unafanya kazi? Mbona unapokuwa na huyo demu, mchumba, rafiki au mke, hawaulizi kwanini unaye? Mbona unapokuwa unaendesha gari hawakuulizi kwanini unaendesha gari au kwanini ulinunua gari?
Hivi aina hii ya maswali hutokana na nini hasa?
Hujamalizia Yasinta,
ReplyDeleteHuyo anayeulizwa kwa nini hivi kwa nini vile, ikiwa ni rafiki yako, wewe nawe unaulizwa, 'rafiki yako mbona hivi na vile?' ukisema hujui, nawe yanakukumba, 'kwa nini humwuulizi?'.
Jamani eee! kwani laizma? mwenyewe akitaka atasema, kwani mtoto mdogo huyo? na isitoshe, kama sina tabia ya kuuliza, kwa nini niulize? hua inaniudhi kweli hii tabia ya kuuliza uliza habari za maisha ya watu, hasa kwa sababu za mtu kutaka kujua tu. Kama sitaki kuuliza mtu asinisumbue ati kaw nini sijui. Na kwa bahati mbaya huwa ninajibu bila kuficha kuwa, SIJUI. Hujamuuliza? HAPANA. Kwa nini? AH NI MAMBO YAKE. (kimoyo moyo nasema, hayanihusu).
Finito!
Mimi nilikuwa naulizwa kwa nini niliamua kuacha chuo na kuwa mjasiriamali?
ReplyDeleteNimekuwa nuikiulizwa hili swali karibu kila siku na hata baadhi ya wanblog wenzangu waliwahi kuniuliza swali hilo.
Kusema kweli haya maswali uliyoyasema dada Yasinta na mengine ambayo hujayaweka humu yamekuwa ni kama sehemu ya mazungumzo yetu ya kila siku, kama hamtaulizana wenyewe basi mtajiuliza kuhusu mtu mwingine.
mimi huwa maswli ya namna hii hayanikeri, k3wani aulizae antaka kujua
Dada Yasinta kwanini unajiuliza?
ReplyDeleteSijui lakini kwanini nakuuliza!:-(
Nadhani ni swali la msingi.
ReplyDeleteHata ulipotaka kublog ulijiuliza KWANINI?
Watanzania tunasifiwa sana kwa kuuliza, mtu unamuulizaswali badala ya kujibu nae anuliza swali....
ReplyDeletekwa nini!?????
Kaluse,
ReplyDelete...(mara nyingine) swali ni jibu. Na swali linakuwa msaada kuliko maelezo yanayoishia na nukta. Ukiulizwa unafikiri. Ukielezwa unaweza usifikiri.
Anyway, ukiacha maswali, sipendi hata majibu ya maisha yasiyonihusu. Kujua habari zisizokuhusu, ni kutafuta matatizo yanayokwepeka.
unaweza kujibu swali kwa njia tatu.
ReplyDeletemosi, unajibu swali kwa swali
pili, unajibu swali kwa mkato
tatu unajibu swali kwa maelezo.
sasa inawezekana wengine hawajui kuwa wanatakiwa kujua kwahiyo waelimishe, na pengine kuna wengine wanajua kuwa wanajua lakini hawataki kuonyesha kuwa wanajua hao wachoyo.
lakini swali kwanini tunakushauri namna ya kujibu au kutojibu swali?
turejee kwa kitururu
Hello Yasinta,
ReplyDeleteFortunately, the worker is lying just to sleep, work in China is very heavy.
Marlow
Good night or early day