Wednesday, April 8, 2009

HERI KWA PASAKA WOTE/GLAD PÅSK ALLA


påskgubben

Påskkäringar

Haya wasomaji naona sasa pasaka inakaribia. Nimeamua niwaeleze kidogo mila na desturi wakati/kipindi hiki cha pasaka huku ninakoishi ni tofauti sana na nyumbani TZ. Ngoja nianze kuwaeleza kuliko kuanza kuwachosha. Ni hivi alhamisi kuu ni kama kawaida au nimesahau sijui yaani watu wanakwenda kazini kama kawaida. Ijumaa kuu baadhi ya watu hawafanyi kazi na JUMAMOSI KUU hapa ndio sikuuu kubwa sio kama nyumbani TZ sikukuu ni jumapili.

Haya sikiliza sasa siku ile ya jumamosi watu wote ni lazima kula mayai kadiri unavyopenda bila mayai basi si pasaka tena. Wana mila hii ya kula mayai kwa sababu hapo zamani kuku waliacha kutaga mayai. Na ghafla walianza tena kutaga na siku ile ya waliyoanza kutaga ilikuwa JUMAMOSI KUU. Hii ndio sababu siku hii ni lazima kuwe na mayai mazani.

Halafu kitu kingine siku hii ya JUMAMOSI KUU watoto wadogo wanavaa kama mababuna mabibi hapo zamani. Pia wanajichora usoni na kalamu za rangi .Na pia wanakuwa na barua ambazo wameziandika/chora wenyewe kwenye vikapu. Na wanapita kila nyumba na kubadilishana na pipi. Ni mila yaani ni kama jambo la kutakiana pasaka njema. Kwa hiyo kipindi kama hiki kila kaya inabidi iwe na pipi au matunda kama huna hivyo viwili basi uwe na hela. mwanzoni nilishangaa lakini sasa nimezoea. HERI KWA PASAKA WOTE!! GLAD PÅSK ALLA!!

9 comments:

  1. si mchezo, hiyo kali kweli kweli ya kuku kususa kutaga na kuanza tena kutaga Jumamosi Kuu. walisusa sijui kwa vile jamaa walikuwa wanawaibia sana mayai. Du, umenikumbusha wakati tupo shule,kulikuwa na utaratibu wa kula mayai kila Jumapili, sasa kuna kipindi kuku walisusa kutaga, basi tukawa tunasema "hii kali kuku na wao wanatumia condoms" ndio maana hawatagi. Kule kwetu Pasaka ni jogoo aliyewika wakati Peter anamkana Yesu.
    Pasaka njema wadau wote.

    ReplyDelete
  2. duh! hao kuku ni noma.
    huku ijumaa kuu no kula nyama wenzetu jumamosi kuu full mayai.
    pasaka njema nawe.

    ReplyDelete
  3. Ama kweli kila jamii ianvisa asili vyake.
    Kuna huku pasaka kwa nyama, ughaibuni pasaka kwa mayai.

    Asiye na jina katoa mpya.
    Duh!! kuku kutumia condoms?
    iyo yahitaji tafakuri.....
    Dada yasinte pasaka nyema pamoja na wadau wote.
    Nisalimie E & C

    ReplyDelete
  4. aisee. sisi tusio na sikukuu tumeungua moto jamani. yaani zote sio zetu isipokuwa kila siku kwangu nikuu kama nyingeyo. basi nitapata muda wa ku-meditate ufukweni mpaka basi.

    ongeleni muabuduo kisichojulikana kwenu, amina

    ReplyDelete
  5. Tamaduni zetu zinatutofautishaje na hawa?

    ReplyDelete
  6. Bwaya kuna tofauti kubwa huoni wenzetu huwa wanajichora pamoja na kula mayai kwa wingi?

    ReplyDelete
  7. Pasaka njema kwa Wote.

    Nitajaribu kujibu swali lako kaka Bwaya, Naona Shabani ameanza kidogo. Nitaendelea:- Tofauti ya hawa ni kweli wanakula mayai mengi na kujichora. Pia wanaamini kuwa rangi ya njano ni rangi/alama kwa Pasaka kwa hiyo ndani ya nyumba kunakuwa na panzia, vitambaa na wengine hata nguo pia zinakuwa za njano. Rangi ya njano inawakilisha maua ya pasaka(påskliljor) mayai na vifanyanga(kuku)

    Pia hapo Zamani za kale kulikuwa na kuamini kuwa kulikuwa na wanawake wachawi(påskkäringar) ambao walikuwa wanasafiri sehemu (ambayo inaitwa Blåkulla) kwa mfagio na wakiwa na birika ya kahawa kwa ajili ya kuomba vitu vizuri au pesa.
    Na halafu JUMAMOSI KUU wanawasha moto (påsksmäll) ili kuwatisha/fukuza wachawi. Kwa Hiyo hii tamaduni/mila bado inaendelea mpaka leo.

    ReplyDelete
  8. Da! Wenzetu hawa wanaua ndege wawili kwa jiwe moja.

    Nawatakieni pasaka njema,
    furahieni kwa kila li'lo jema,
    mamisosi kujichana,
    furaha mpaka jua li'tapo zama,
    waso'jiweza kuwatazama,
    nao maisha kufurahia.

    Niwatakie Paska njeeeema!

    ReplyDelete
  9. Samahani nilisahau kusema na hayo mayai yanakuwa yamechemshwa.

    ReplyDelete