Friday, April 3, 2009

Video documentary : Taifa linalojengwa na wafanyakazi wa majumbani

Nimeichukua kwa Da Subi kwani najua kuwa wote tuna nia moja.





Nikiwa kama mzazi nimeguswa sana na maelezo katika vido hii kwa kweli ni dhurumana pia naweza kusema unyama kabisa. Soma na sikilizeni wenyewe na semeni mnawanza nini na je huu ni uungwana?

Ni imani yangu kuwa hakuna ubishi ya kuwa elimu ya darasani yenye malengo maridhawa ndiyo msingi mahsusi wa maarifa na maendeleo kwa jamii yoyote ile. Mtizamo huu ndiyo unaonisababisha nisikubaliane na kitendo cha watoto kufanyishwa kazi majumbani kwa kisingizio tu cha kuwa mzigo kwa kushindwa kuendelea na masomo ama ya sekondari au ufundi.

Kazi si adhabu wala dhambi, lakini kazi yenyewe inapofanyika bila kuzingatia mustakabali wa maisha ya wafanyakazi wenyewe, hasara inayopatikana kwa muda uliopotea na kudumaa mawazo ni kubwa kwa wahusika pamoja na Taifa lao. Nchi inakosa kuwa na raia walioelimika kwa kiwango cha kutosha kuchangia katika uchumi wa Taifa lenyewe.

Nadhani, nchi inayojengwa kwa vibarua na ufanyakazi wa huduma za nyumbani haiwezi kuwa na misingi imara katika mipango ya maendeleo. Mtapanga vipi mipango ya maendeleo ikiwa unaopanga nao wanafahamu shughuli za nyumbani tu? Ikiwa uamuzi wetu ni kusema habari ya maendeleo lakini hatuna nia ya kuendelea, basi hakuna sababu ya kuzungumzia mipango ya maendeleo, tuendelee kuishi hivi hivi tu. Lengo letu likiwa ni kuendelea, basi ni dhahiri kuwa inatubidi kubadilisha mifumo yetu na kuachana na kuendelea kufanya shughuli zile zile hasa zisizo za ushindani wa kimataifa huku tukitaraji kuona mabadiliko ya kutufikisha kwenye kilele cha maendeleo.

Kwa kweli tumebakia kuwa Taifa la wapokeaji na watendaji wa mazoea badala ya kuwa Taifa lenye wajuzi na wafikiriaji wa mambo mbadala. Hii haifai.
Film documentary hii inaonesha na kuelezea maisha ya watoto wanaofanya vibarua majumbani.

8 comments:

  1. Nimeiangalia hii video. Inasikitisha, lakini ni kioo cha jamii yetu, kinachomulika yanayofichwa. Video hii ni muhimu kwa kufundishia hali halisi ya jamii yetu. Labda wengi wakiiona wataweza kuguswa wakaanza mkakati wa kuleta mabadiliko.

    ReplyDelete
  2. inasikitisha sana kwa kweli.

    ReplyDelete
  3. Nimesikitika sana.
    kama utakumbuka niliwahi kuandika habari ya hawa ma house girl na madhila yao.
    Shukrani kwako na kwa dada Subi kwa kukumbushia hili.

    ReplyDelete
  4. nahisi hii haitapata comment nyingi kwa vile wengi wetu inatukumba, majumbani kwetu tuna hawa mahousi girl na hatuwafanyi kuwa kama sehemu ya familia zetu, wanalea wanetu lakini tunawaona ni kama vitu fulani tu, hatuwapi umuhimu fulani katika nyumba zetu.

    ReplyDelete
  5. DA YASINTA HIVI HUYU ASIYE NA JINA NI NANI!!!!!!!!!!???????

    ReplyDelete
  6. Prof. Mbele,Kama nilivyosema nikiwa mzazi na pia mwanamke kwa kweli nimeguswa sana kuona bado watu wengine wanatutesa, kutunyanyasa na pia kupigwa namna hii.

    We usiye na jina ndiyo inasikitisha kweli
    Koero, Asante Ila kwa kweli kuna wanaume wakatili sana kweli anathubuthu kumweka mtu alale na mbuzi,

    We usiye na jina una maana gani kusema hivyo????

    Koero hata sijui ni nani kwa kweli

    ReplyDelete
  7. duh! ni kweli haya ndiyo yanayotokea.
    wakati nikisoma kuliandaliwa mdahalo uliokuwa ukijadili ajira kwa watoto na mkazo ulikuwa ajira za uhousegirl. nakumbuka mwanafunzi mwenzangu alimchallenge mwalimu wa kike aliyekuwa ameandaa mdahalo huo kuwa anapiga kampeni dhidi ya huu unyanyasaji wa watoto wa kike ilhali kwake ana housegirl anaeteseka pia. sijui nini maana yake. lakini Mahatma Ghandhi alisisitiza 'u must be the changes you wish to see in the world'
    sisi tulio na mahousegirl majumbani tunapaswa kuwa wa kwanza kuwakomboa.
    kiukweli inasikitisha sana tena mno.
    ni hayo tu!

    ReplyDelete
  8. Very interesting opportunity of housegirls, cooperation to overcome the difficulties it is very important, my dream is that finally the African continent and all the people with difficulty, can one day be happy and serene.

    But unfortunately that day is far away.

    Hello Yasinta, a hug Marlow

    ReplyDelete