Mungu nakuomba unisaidie niwakumbuke wenye njaa ninapokuwa na chakula, wagonjwa nianpokuwa na afya nzuri, wote wanaoteseka kwa sababu ya vita ninapokuwa na amani, wasio na nyumba ninapokuwa nimelala na pia kuwa ndani ya nyumba yenye joto, pia nakuomba unisaidia niwakumbuke yatima kila ninapokuwa na wazazi wangu.
Na pia nakuomba:
Bikira Maria mama wa msaada na uibariki familia yangu, kaka zangu, dada zangu, wazazi wangu na watu wote dunia hii katika dhambi: AMINA
Ahsante sana da Yasinta kwa kutukumbuka na kututakia Jumapili njema. Nami naungana nawe kuwatakia ndugu zetu Jumapili njema.
ReplyDeleteTukumbuke kuwaombea wale wenye uhitaji, wanaosumbuliwa na maradhi, njaa, kunyanyaswa na kadhia zote.
Pia tuwaombee wale wenye ujasiri wa kunyanyasa wengine, kudhulumu wengine, kuwaumiza wengine. Wale wenye ujasiri wa kuzungumza wakijawa na nyuso za tabasamu huku wakitambua kuwa kuna watu wanaumia ilhali wao hawajatimiza wajibu wao kuzuia hayo.
Tuombe kuhusu mambo mengi sana. Lakini kubwa zaidi tuombee amani na furaha na matumaini na upendo mioyoni mwa watu wote. Tuombe ili dunia pawe pahala salama.
Tuombeane tuyashinde mapungufu yetu.
Amina.
Ahsante kwa sala nzuri,
ReplyDeleteJumapili ya leo imekuwa si nzuri sana kwangu, juzi nilikuwa mwezeshaji kwenye mjadala fulani wa kitaaluma.
Kutokana na kuongea kwa muda mrefu koo langu limepata mushkeli na hivyo kuniletea homa.
Hata hivyo baada ya kusoma Sala yako nimepata nafuu.
kaluse unamaanisha ungesoma sala hii kabla ya kuingia kwenye mjadala huo, koo lisingeuma?
ReplyDeleteda yasinta kwa nn tumwombe bikra maria na ni kwanini anaitwa bikra japo alizalishwa? sio bikra tena huyu!
Usengwili sana Yasinta, sala ya bwina sana, Domika ya lelu nipatili amani ya mahele sana, ndava ya sala yaku. Ujovili chakaka sana timuwombaya mahu Bikira Maria atiwombelahi kwa mwana waki, wasalimilahi wajomba vangu kutali huko.
ReplyDeleteNgalilihina.
Asante Da Yasinta kwa kutuombea na kututakia siku njema. Nawe pia uwe na wakati mzuri na wale wenye taabu a mihangaiko pia wawezeshwe kulingana na imani zao.
ReplyDeleteKila la kheri kwa wote na mwanzo mwema wa wiki ijayo.
Blessings
DU NILIKUWA SIJAONA, KUMBE UMEWEKA PICHA NYINGINE!!
ReplyDeleteUMEPENDEZAAAA!!!!!!!!!!
Fadhy, shabani, kamala, mzee wa changamoto na wewe usiye na jina asanteni sana kwa maoni yeni.
ReplyDeleteShabani asante kwa kuipenda picha yangu hiyo nimepiga jana.
aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaah acheni hizo na MIMI nisiye na jumapili mwana wa afrika nifanyeje. mmmm nimegundua kitu KWAHERIIIIIIIIII
ReplyDelete