Ebu angalieni hapa halafu fananisha na hapo juu. Maisha ya kuku hayaachani sana na ya binadamu. Kwani kuku ana bahati yeye anaatamia mayai wiki kama tatu hivi. Hapo tayari anatotoa vifaranga na atavitunza na kuvilinda na maadui wabaya kama vile mwewe na kadhalika. Baadaye wakiwa wakubwa anawadonoa hapo ndio kuwaambia SAMAHANI sasa muda umefika kwa ninyi kujitegemea.
Jamani sikujua hata kukuanakuwa mkali kwa watoto wake angalia hapo hizo ndita zilivyosimama.
ReplyDeleteHa ha haa, leo nimecheka kupitia blogu ya Yasinta, ha ha ha, ati kuku anasema, 'SAMAHANI sasa muda umefika kwa ninyi kujitegemea' ha haa ha, Yasinta, unaweza kusikilizana na kuku?
ReplyDeleteYasinta leo ni mara yangu ya kwanza kufika kwenye blogu yako. Nimekua nikikusoma maoni yako kwenye blogu za Lazarus, Pilikapilika, akina kaka Michuzi, ChangamotoYetu nk lakini sikufahamu kuwa unablogu. Basi nimeongeza blogu yako kwenye orodha yangu ya blogu rafiki.
Ufanikiwe!
Asante sana dada Subi.kuhusu kuku anapowaambia watoto wake wajitegemee ni pale anapowadonoa kwa sababu yeye sasa anataka kutafuta au niseme kuanza kutaga tena. Sijui kama nimeeleweka. Karibu sana na tena na tena.
ReplyDelete