Kupenda/upendo ni kitu cha ajabu sana mara nyingi nimekuwa nimejiuliza kwa nini sisi binadamu tuna upendo tofaoti kwa kila mtu. Nikisema hivi nina maana kuna wakati mtu inaweza kutokea unampenda mtu kiasi kwamba huwezi kujizuia. Na cha ajabu mara nyingine uanaweza kumpenda mtu ambaye hujawahi kumwona ana kwa ana(uso kwa uso) na upendo ukawa wa nguvu kali sana.
Halafu sasa inaweza kuwa kinyume kabisa. Yaani watu tunaweza kuwa na chuki. Unaonana na mtu siku moja tu na utasikia simpendi kabisa jamaa huyu. Au hata kuangalia tu picha yake unapatwa na chuki. Nashangaa sana kwa uwezo kama huu ambao MUNGU amatupa na pia SHETANI anaingilia na kuharibu.Swali:- Hivi hii inatokana na nini?
hayayayayayya. sisi sote ni kitu kimoja na kumchukia mwingine ni kujichukia mwenyewe au kumchukia Mungu aliyemuumba. kimsingi kupenda ni laizma natunamfikia Mungu kwa njia ya upendo sio kumpenda binadamu pekee bali viumbe vyote a.k.a kazi ya mikono yake.
ReplyDeletekumchukia mwenzio kwa sababu yoyote ile ni uchizi na ujinga.
sawa lakini kuna watu wanachukia waenzao kiasi kwamba anaweza hata kuua
ReplyDeletetunahitaji kufanya utafiti au tuwaombe wataalamu wa sosholojia watwambie kulikoni hali hii.
ReplyDeletekwa nini mpaka kwenda sosholojia kwani huwezi tu kujirekebisha mwenyewe?
ReplyDelete