Wednesday, September 3, 2008

HÖST= AUTUMN MAJIRA YA KUPUKUTIKA KWA MAJANI

Mmmh! Sasa mapambano yameanza, yaani hapa Sweden kwa sasa ni majira ya baridi, kupukutika majani. Kuna upepo, baridi, mvua, jua kidogo halafu giza pia limeanza kuingia mapema kidogo.

Huwezi kuamini miezi mitatu iliyopita kulikuwa kunapendeza sana maua mazuri na joto kali kama Bongo. Yaani watu tulikuwa tunavaa nguo nyepesi na kandambili au pekupeku. Lakini sasa mmh haiwezekani ni lazima kuvaa sweta nzito na pia viatu(raba) kusema kweli kipindi hiki natamani sana kuwa Tz.

Na ni wakati huu watu wengi wanapata mafua na pia kukoho. Na hapa ni mwanzo tu, baadaye ndo itakuwa kazi zaidi, ambayo inanichosha sana yaani kuvaa koti kubwa, soksi, viatu vizito, kofia na glavu(glove) Hapo ndo mtu unapoonekana mnene kama tembo. Mmmh! Maisha kazi kweli

No comments:

Post a Comment