Saturday, September 20, 2008

MKOA WA RUVUMA

Leo nmeamua kutembelea Ruvuma kijiografia na Historia fupi.

Mkoa wa Ruvuma ni kati ya mikoa 26 ya Tanzania. Mkoa huu umepewa jina kutokana na mto Ruvuma ambao ni mpaka wake upande wa kusini ni Msumbiji, upande wa magharibi umepakana na ziwa Nyasa na mkoa wa Morogoro, upande wa kaskazini umepakana na mkoa wa Iringa na Lindi na upande wa mashariki umepakana na mkoa wa Mtwara.

Katika Mkoa wa Ruvuma kuna mikoa mitano:- Songea mjini na wakazi wake ni 131,336, Songea vijijini ina wakazi 147, 924, Tunduru ina wakazi 247, 976, Mbinga ina wakazi 404,799 na mwisho Namtumbo wakazi wake ni 185,131.
Songea ni makao makuu ya mkoa kwa hiyo jumla ya wakazi wa mkoa wa Ruvuma ni 1,117,166 (sensa 2002) Makabila makubwa katika mkoa wa Ruvuma ni Wayao, Wangoni, Wamatengo, Wandendeule na wandengereko.

SONGEA
Jina Songea ni kumbukumbu ya Chifu Songea wa wangoni, aliyekuwa na Ikulu pale wakati wa kuenea kwa ukoloni wa Ujerumani akauawa na Wajerumani, wakati wa vita ya majimaji.
Mji wa Songea wakati ule iliandikwa Ssongea, mji huu ulianzishwa mwaka 1897 kama kituo cha kijeshi cha kijerumani.
Mazingira ya mji yaliathiriwa vibaya na viya ya majimaji na ukandamizaji wake na Wajerumani.
Songea ikaendelea kuwa makao makuu ya mkoa wakati wa utawala wa Uingereza katika Tanganyika na baada ya uhuru katika Tanzania huria.

1 comment:

  1. Asante kwa kutupa taarifa za mkoa wa Ruvuma inaonekana Geografia haikucheza mbali nawe

    ReplyDelete