Mmh! sijui nianze vipi? Haya basi naanza hivi:-
Wote nadhani mnajua mzunguko wa masiha. Nina maana jinsi ya kuishi na watu wa aina mbalimbali. Kama niyi hamjaishi hivyo basi mimi nimeishi, Wote mnajua nimezaliwa kijiji kimoja kiitwacho Lundo,(Wanyasa) nimeishi pale mpaka mwaka 1985, baada ya hapo tukahamia kijiji cha kingoli (Wangoni) pale niliishi mpaka nilipomaliza darasa la saba. Baadaye nilihamia Songea kusoma, wakati huu familia yangu walihama tena walihamia kijiji cha Mahumbato (Wamatengoni) na baadaye kijiji cha Mdunduwalo nje kidogo ya Peramiho na (wangoni tena) Baada ya masomo yangu nikaanza kujitegemea nikaoangiwa kijiji cha Matetereka(Wilima sec) (Wabena) nikawa pale miaka mitatu na baadaye nikaja huku mbali kabisa Sweden (Waswidi)
Mara nyingine sijui mimi ni nani,na wapi ni nyumbani . Ooh najua mtajiuliza kwa nini kuhama mara zote hizo. Ndiyo baba alikuwa Mwl.
Mmh mwenga gendani ulolayi= Tembea uone. Kazi kweli kweli.
maisha ni safari ndefu hatujui mbele kukoje, kwani wale ulioishi nao zamani mkikutana halafu ukawaambia karibuni nyumbani hakika watashangaa kwani waliokutesa na waliokuona huna faida wataanza kukuona malighafi. lakini ni utamu sana kujifunza
ReplyDeletesi uongo kwani sasa hivi napata sana shida kila mtu anakuja na kujifanya eti anakuja kunitaka hali.
ReplyDelete