Tuesday, August 26, 2008

AGOSTI 26,2008 MIMI NIKIWA NAISHI KINGOLI/LITUMBADYOSI

Binadamu tuko tofauti kuna wengine wanasahau upesi na wengine kama mimi. Ni hivi kuna jambo moja, ambalo mimi SITALISAHAU nilikuwa miaka 10 labda. Baba na mama walikwenda hospital Litembo. Na mimi na kaka zangu tulibaki kwa (babu) baba mkubwa. Huyu baba mkubwa alikuwa na watoto wa kike 6 na huyu mkubwa aliitwa Maria. Siku moja jumapili;- Nilimwomba dada Maria kanga kwani mimi nilikuwa sina ALININYIMA na kuniambia kwa nini baba yangu ambaye ni mwalimu asininnunulie. Kwani wakati ule nilikuwa mtoto wa kike peke yangu. Naye alisema, upo peke yako mtoto wa kike na wazazi wako wanashindwa hata kukununulia kanga.(Mwana mdala nga veve vishindwa kukugulila nyula).Kilugha Siku ile nililia sana, mpaka sasa roho bado inaniuma. Sikujua kama binadamu wanaweza kuwa wakatiri kiasi hiki, na hasa ukizingatia yeye alikuwa dada yangu. Kwa mimi ni vigumu kuelewa. Tokea siku ile sijawa na mawasiliano naye natumaini hata yeye anakumbuka alinifanyia nini. Lakini sidhani kwani waswahili wanasema mtendaji hakumbuki ila mtendewa ndiye anayekumbuka. Mimi ni mtu mmoja ambaye kwa ujumla ni mvivu. Nina maana kuhusu mambo ya kazi ngumu hasa nilipokuwa mdogo.Kule kingoli maisha yalikuwa magumu kulima mpunga na pia karanga na mihogo. Nakumbuka kila wakati mimi nilikuwa wa mwisho wakati tulikuwa shambani.Yaani walikuwa wananiachia/ruka matuta.Mazao ambalo tulikuwa tunalima sana ni karanga na mpunga tangu asubuhi mpaka mchana. Halafu kule kingoli tulikuwa tunakula sana ugali wa muhogo na kwa kuwa sisi tulihamia kule, tulikuwa hatuna shamba la mihogo. Kwa maana hiyo ilibidi tununue, ndugu yangu huko tulikonununu kulikuwa mbali mnatembe mpaka miguu inauma. Tulikuwa tunachimba, kumenya kabisa ili uzito upungue. Baada ya hapo kurudi na mzigo kichwani na jua linawaka. Kufika nyumbani kutua mzigo, kuandaa chakula cha mchana na kula. Kupumzika kidogo kisha kuanza kazi ya kuchotelea maji ya kulowekea ile mihogo. Kwani kulikuwa hakuna maji ya bomba, tulikuwa tunachota kisimani. Jamani kweli maisha ni safari ndefu, nina maana kuna watu wengine hawatanielewa nini ninachokisema. Kwa kusema kweli maisha yangu hayajawa afadhali nimeendelea kuteseka mpaka leo. Nadhani mungu alipanga niwe mtu wa mateso mpaka siku ya mwisho.

2 comments:

  1. kwanza pole na hongera kwa uliyopitia.Hongera nikiamini yamekufanya uwe jasiri leo na mwalimu wa wengi.

    Pole ni moja ya mitihani migumu ya maisha.

    kikubwa jitahidi kuamini kila linalomkuta mwanadamu linatokea kwa malengo yake.

    Kubwa ya yote napenda sana mfumo wa uandishi wako."house stlye" nzuri.

    Unafahamu pombe inaitwa myakaya?Niliwahi kufika Ruvuma na kukaa miezi 3 kikazi.

    Nilijifunza mengi na kupata marafiki wengi.Kikubwa nilifurahi sana sana kukanya ardgi ya peramiho.Kwani kipindi nipo seminari nimesoma vitabu vingi vilivyochapishwa peramio.

    Nilikuwa sausage za huko,niliona saa ya kihistoria na madhari mazuri.

    Nakumbuka kunyumba...aaa aa

    ReplyDelete
  2. asante, ndiyo najua myakaya ni nini ila sinywi pia unajua kuna komuni pia halafu ulanzi je ulikunywa. KARIBU TENA RUVUMA Peramiho

    ReplyDelete