Friday, August 22, 2008

AGOSTI 22,2008 ERIK NA YASINTA KATIKA MAZOEZI YA KUKIMBIA


Leo nimeamua kumchukua na kijana wangu kwenda kufanya mazoezi ya kukimbia tukiwa tumevalia T-shirt za kutoka TZ. Je? unafikiri nani alimshinda nani. Kuna zawadi inamsubiri atayejibu vizuri.

7 comments:

  1. Kwanza hongera sana kwa kufanya mazoez ya kukimmbia tena na mwanao maana unamlea vizuri.

    Ila nina uhakika Eric alikuacha mbali sana nahisi yeye alipokuwa Songea wewe ulikuwa bado upo Njombe unahema tu.

    Kwa kweli 2012 olympics in London lazima Eric atuwakilishe, yaani watanzania tunashindwa hata kuruka long jump, kutupa mkuki? kulenga shabaha, hata wale wa nyasa wameshindwa ku Kayak jamani?
    Nimesikitika sana kwa Tanzania kukosa medali hata moja ila naamini Nyumbani Tanzania tunazo dhahabu nyingi labda ndo maana viongozi hawataki twende China tukashindane na badala yake tugawene dhahabu tunazochimba wenyewe.

    ReplyDelete
  2. Hivi Erik ana miaka mingapi, sijui naangalia vibaya ila naona kama yeye ni mrefu kuliko mama yake?

    Labda macho yangu hayaoni vizuri

    Sijui!

    ReplyDelete
  3. hapana huna tatizo la macho ila mimi nilipiga magoti na yeye alisimama kwenye ngazi. Erik ana miaka 8

    ReplyDelete
  4. Jamani acheni tu yaani nipo hoi kabisa juzi nimecheza mpira{nimeamua kurejesha enzi zangu za kandanda,kiungo mkabaji,kiungo mshambuliaji/beki wa kati na kulia}nakwambia mapaja,kiuno,meno na kila kitu kinauma.Nimeapa kwamba sasa naanza mazoezi makali sana nitakuwa na kasi kama ya Usain Bolt olipmiki ijayo medali kumi za dhahabu katika kuvua samaki,kutega nyavu,kupalaza mtumbwi,kuogelea,kuranda nyavu,kuoposha madongo,kukong'ondela n.k lakini nimeudhika sana yaani hata tufe hatujui,kuogelea?utakuta pale mlimani chuoni mashindano ya kuogelea huku waogeleaji wenyewe mbavu mbili msuli wa kuazima pumzi bakuli mmmh!!! olimpiki ijayo nakusanya wanyasa kibao lakini tutakimbia pekupeku kama kaka Mbilinyi afanyavyo kuwafunza wale wadogo zangu.Jamani Bolt na Powell ni binadamu wa wenye kasi ya ajabu au?vipi yule Dibaba dada kutoka Ethiopia anapumzi nyingi nahisi amechanjia mzizi wa muarobaini au lupocho?{mtabisha mtasema nimeanza kuwanga na uchawi mgongoni mtajiju}nawaambia Erik na Yasinta hamniwezi sasa ninakimbia kama Bolt nguvu kama Josia Thungwane{mnakumbuka olimpiki ya 1996?} mkimbiaji toka kwa mandela huyu jamani ilikuwa balaa tupu. mmmh siyo kwamba sifanyi mazoezi bali nataka kuanza na mpira kwanza halafu nishindane na Yasinta...njo unione nyasa hapa.Olimpiki ijayo nashiriki hata kuogelea halafu nyie waongo hebu oneni mnaita mitindo huru{free style}katika kuogelea pale nia yenu nini kunikomoa mnyasa?

    ReplyDelete
  5. Kaka Mpangala Umenivunja mbavu ile mbaya.
    Pia nakupongeza sana kwa kuandaa kikosi kamili cha kuleta medali za dhahabu London Olympic 2012.
    Kwa kweli inabidi tuungane tutengeneneze kikosi kamili cha Olympic.
    Mimi nashindwa kuamini kama watanzania tunaweza kukosa medali za kuruka long jump, au kurisha mkuki au kuogelea au kukimbiza hivyo vimtumbwi (Kayak) yaani hata kurusha mawe (tufe) hatuwezi jamani, sasa mawaziri walienda kufanya nini? 2012 kaka Mpangala tupeke na sisi kikosi chetu, nipo pamoja na wewe na dada Yasinta wewe utasimamia riadha lazima Dibaba tumpige chini.

    ReplyDelete
  6. Mi ngoja tu nitoe jibu ingawa ninamshaka sana kama nitapewa zawadi.Mashaka yangu yanakuja hasa mto zawadi naye ni mshiriki...aaa aaa ..kinyozi hajinyoi.


    Yap inapendeza sana kufanya mazoezi japo kajasho katoke mzunguko wa damu baada ya mapigo ya moyo kwenda fasta....aaaa

    siku njema

    ReplyDelete
  7. nyie mbona mnaniongezea mahanjamu ya kusaka tiketi ya olimpiki ijayo London? ngoja jambo la kwanza ni kuwasiliana na mzee wangu Fred Macha wa kitoto blogu,halafu namwambia aandae gheto la kufikia siyo hoteli za kitalii wala sitaki kusikia kwani wali unakaa first in lat out majuma saba halafu useme umepikwa sasa hivi. najua ataandaa samaki na kisamvu bila kusahau mlenda ambao utanifanya niwe mwepesi kuzidi kasi ya Bolt. jamani Jamaika toka Black Bamboo hadi riadha? mnasemaje hapo?

    ReplyDelete