Wednesday, July 9, 2008

JULAI 9, 2008 KWA NINI

Nimekuwa najiuliza kila siku kwa nini binadamu tumezaliwa tofauti. Labda kwa namna nyingine ni afadhali. Angalia kama wote tungezaliwa na hasira, chuki, haraka n.k dunia ingekuwaje? Na je? kama wote tungezaliwa wenye furaha, upendo, huruma n.k ingekuwa si vizuri. Kwani katika maisha ni muhimu sana kupendana, sisemi ni lazima kupendana hapana kwani hili linakuja lenyewe( ni nature kumpenda mtu)

Pia jambo jingine kuwezakusameheana ni muhimu sana hata kama si jambo nzuri inabidi kujaribu. Kwani tusipofanya hivyo tutaishi maisha yetu yote tukiwa hatuna raha. bad feeling) na hii si nzuri kwa maisha ya binadamu.

Chuki na hasira ni muhimu kuviepuka kwani vinaweza kusabisha kifo. Nadhani wote tunajua tukiwa na chuki au hasira matokeo yake ni kuua au kufa. Tumeona watu wakiwa na hasira wanatuma kama pipa la pombe na mwisho wake kifo.

Kuomba radhi na kusameheana sio kitu rahisi na sio wengi wanaoweza ni kipaji. Sijui kama wasomaji mnakubaliana nami????????????????????????????????????

3 comments:

  1. jamani kuna mambo yapo kama yalivyo lakini yanatatiza.kwanini binadamu walikuwa na hasira au chuki,ziliwekwa kwaajili gani?Ina maana mungu aliweka hasira na chuki kwa wanadamu ilitukosee?mbona sielewi.Mmm kweli dada kusamehe ni kipaji inahitaji hekima na uelewa wa hali juu kumiliki hekima yenyewe....nimejieleza vizuri au

    ReplyDelete
  2. Umeghusia jambo muhimu sana kuhusu kusameheana. Hivi karibuni nilikuwa nasikiliza Radio Japani Idhaa ya Kiswahili iliyokuwa ikimhoji mwanamuziki Jean Paul Samputu Kutoka Rwanda.

    Mwanamuziki huyu, ambaye alipitia majanga ya kutisha ya mauaji ya halaiki nchini Rwanda mwaka 1994, hivi sasa anaizunguka dunia akieneza ujumbe wa amani na maridhiano kupitia muziki wake.

    Mwamuziki huyu alipoteza familia yake wakati wa mauaji ya halaiki nchini Rwanda ameamua siyo tuu kumsamehe bali pia kushirikisha rafiki wake wa utotoni alihusika kuiuwa familia yake katika kampeni duniani kuhusu kusameheana.

    Hili linigusa sana nikaamua kuandika article iitwayo "Muziki kama chombo cha amani na maridhiano" ambayo inapatikana: http://bongoline.com/blogs/2/16/muziki-kama-chombo-cha-amani-na-maridhiano.

    Namshukuru sana Yasinta Ngonyani nileyem-quote kwenye article yangu.

    ReplyDelete