Mwenzenu leo nimeenda mpaka nyasa kuvua samaki bahati mbaya kulikuwa na zoruba kwa hiyo nimepata samaki moja tu na huyu amekuwa mlo wa jioni hii. Halafu tena nimekosa unga wa muhogo kwa hiyo nimekula na viazi vya kuchemsha (matosani) najua wengine wanaona wivu sana kazi kwenu. Mmmmmm utamu mpaka kwenye kidole gumba. Nakuomba Mr Mpangala watajie jina la samaki huyu kwani nimesahau kidogo.
Siku nyingine ukienda kuvua samaki Nyasa usisahau unga wa muhogo maana ukizoea unaweza kusahau kuchukua appetite piana ikawa balaa.
ReplyDeleteNatamani sana kuona huo mlo wa samaki na matosani kwani hata matosani yenyewe yana mapishi mbalimbali kuna kuyachemsha (mahelula) kuna kuyapika(futali) kuna kuyachanganya na unga wa mahindi au ngano (kitwangwa) nk.
Je, wewe ulipika vipi?
Nimefurahi!
Nilichemsha tu kakangu. Na ndiyo sitasahau unga wa muhhogo asante kwa kunikumbusha
ReplyDeleteMmmh utwajua tu kwamba hawa watu wanafakamia sana viazi.Lakini kweli utani sana .mimi siyo mpenzi wa futari ya viazi napenda sana kama ulichemsha yaani unanikuna sana hata hivyo mimi sifa yangu ya kwanza kula yaani nakula usipime.kama umechesha kidogo naanzisha varangati au nakwambia sijashiba kabisaaaaaaaa

ReplyDeleteSamaki watamu sana ila sisi ambao tuko Dar tunauziwa kwa bei kubwa utafikiri unanunua mbuzi wa kienyeji na hii ndio maana tunasakamia kila siku dagaa kamba na pwazi, natamani siku moja niwe kijijini kwa babu yangu huko kwimba nikale sangara
ReplyDelete