Wednesday, July 16, 2008

JULAI 16,2008 WASICHANA NA TAHADHARI

Ngoja niachane na picha na niandike kidogo kwani kila siku nilikuwa nawaza nianza vipi sasa nimejua. Ni kwamba nataka kuandika kuhusu maisha ya wasichana:


NI hivi kila kitu hapa duniani kina upande wake mwema na mbaya. Hali kadhalika mawazo na matendo ya msichana/wasichana nayo. Mara nyingi mawazoni mwake/mwao msichana/wasichan hujishughulisha na mambo madogomadogo sana. Kwa ajili ya kujihusisha kwake na hayo mambo madogomadogo hushindwa kuyatekeleza makubwa, mapaswa yake halisi, yenye kuhitaji juhudi kubwa. Hapo hufanana na mtu ambaye anayehangaika kuwaandalia wageni vyakula hali hajawaalika, wala hata hafahamu kama watakuwa watu wa aina gani?

Msichana/wasichana huchukizwa upesi hata kama jambo ni dogo kabisa. Matokeo yake ni manungĂșniko, kutokuwa na furaha, kujaa uchungu moyoni, kujiona ameachwa na jamaa, ndugu, marafiki zake wote. Atajisikia kuwa katika dibwi kubwa la giza. Na hapo inawezekana ni jambo dogo tu. Ikiwa aliyemchukiza ni mama yake, hapo kuna hatari ya kupoteza imani yake kwa mama huyo katika mambo yote. Atasahau upendo wa mamake jinsi alivyomhangaikia na jinsi anavyozidi kumhangaikia hata leo hii. Hii yote ni ajili ya chuki. Kwa hiyo mwisho wake unakuwa msichana huyo anaanza kutafuta kitulizo nacho ni mvulana. Kutokana na hasira msichana huyo anaweza kumpokea mvulana yeyote bila hata kumchunguza dhahiri.

Kwa sababu hiyo ni hatari kwa msichana huyo kujihusisha na mvulana kwa ajili ya fadhila moja tu aliyoiona. Ndani ya fadhila kuna huruma,ukarimu na wema. Anasahau kabisa kudadisi na pia kuzungumza lengo halisi la urafiki huo. Anakuwa hajali tena kuchunguza ya kuwa urafiki huo ni wa kumhatarisha ama la.
Yawezekana upendo huo umesukumwa na tamaa za kimwili tu, hivyo kwamba hata watafunga ndoa itavunjika ila sasa kwa vile hakupima kwa uzito wa mambo, msichana anakuwa anajiingiza katika ndoa kipofu ni kama kipofu mwenyewe aingiapo hatarini. Kutokana na msukumo huo na kwa ajili ya maumbile yake kuna hatari msichana huyo asikubali ushauri wa wazazi wake, jamaa, marafiki au hata wakubwa wa kanisa. Uamuzi wa aina hiyo huhatarisha sio tu ujana wake bali hata maisha yake yote ya siku za mbele

2 comments:

  1. Ndugu msichana hapa cha kufanya ni kwamba acha mambo madogo madogo yasije yakakuondelea utulivu na amani yako ya moyoni. Pia usikubali kwa kama bendera upeperushwe na mawimbi ya upepo tu. Tawala tamaa zako za kibinadamu, na usikubali kushusha hekima yako

    ReplyDelete
  2. Nafikiria nini hasa kinapelekea masuala haya kwa wanawake.mara nyingi nimekuwa nikijisaili kwamba kwanini mambo yapo kama yalivyo au kuona wanawake njia zao za kutuliza hasira/chuki ni wavulana.Ni mara ngapi hawa wanaweza kuishi bila wavulana.Lakini twaweza kunena na kuenenda njia zisizo na mbigili ili tuweze kuwa na maisha mema.Lakini suluhu ni wavulana?kwanini yatokee kwa wanawake tu?Inakuwaje haya yakawa kwa wanawake pekee?Haaa hivi nimejieleza vema.Mwanamke lazima abadilike na kuona anaweza kuishi kama yeye na siyo kutegemea nguvu za mwanaume au hisani za kuwawezesha,lazima apange kuwa kama yeye vinginevyo yaleyale.mm ngoja nikomee hapa

    ReplyDelete