Monday, February 25, 2008

watoto afrika na watoto ulaya

Tembea uone! kutunza watoto ni kitu ambacho wengi wanafikiri ni rahisi au nisema kila mtu anaufanya urahisi au ugumu mwenyewe. Kwa vile sasa nimeishi nchi mbili tofauti nimeona pia jinsi wazazi wanavyotuza watoto wao. Kwa mfano watoto Tanzania wanafunzwa kujitegeme wangali wakiwa miaka 7 kama hivi wanaweza kutengeneza chakula, kutunza wadogo zake kama anao. Yaani zile kazi ndogondogo zote za nyumbani. Na sasa nipo hapa Swedeni miaka mingi kidogo naona watoto jinsi wanavyotunzwa/dekezwa. Watoto wana vifaa vingi vya kuchezea na pia vitu vingine havina maana kabisa. Mtoto miaka 10 au zaidi hawezi kujiandalia chakula anasubiri mama amwandalie. Binafsi najaribu kuwalea watoto wangu utamaduni wa nchi zote, ila ni ngumu kidogo kumfundisha mtu utamaduni wa Tz wakati upo Swedeni.

1 comment:

  1. kilea watoto katika tamaduni hizo inahitaji uangalifu mkubwa kwani unaweza kujikuta ukaunia moyo kwa kuwa hukulelewa katika muundo huo wa maisha lakini polepole tutafika tu.Walee vizuri wajithamini na kujivunia malezi ya wazazi kama nyie

    www.lundunyasa.blogspot.com
    Markus

    ReplyDelete