Monday, February 25, 2008

watoto afrika na watoto ulaya

Tembea uone! kutunza watoto ni kitu ambacho wengi wanafikiri ni rahisi au nisema kila mtu anaufanya urahisi au ugumu mwenyewe. Kwa vile sasa nimeishi nchi mbili tofauti nimeona pia jinsi wazazi wanavyotuza watoto wao. Kwa mfano watoto Tanzania wanafunzwa kujitegeme wangali wakiwa miaka 7 kama hivi wanaweza kutengeneza chakula, kutunza wadogo zake kama anao. Yaani zile kazi ndogondogo zote za nyumbani. Na sasa nipo hapa Swedeni miaka mingi kidogo naona watoto jinsi wanavyotunzwa/dekezwa. Watoto wana vifaa vingi vya kuchezea na pia vitu vingine havina maana kabisa. Mtoto miaka 10 au zaidi hawezi kujiandalia chakula anasubiri mama amwandalie. Binafsi najaribu kuwalea watoto wangu utamaduni wa nchi zote, ila ni ngumu kidogo kumfundisha mtu utamaduni wa Tz wakati upo Swedeni.

Saturday, February 23, 2008

ruhuwiko 23/2 jumamosi

Habari zenu ndugu wasomaji hii ni blog yangu ya kwanza. leo mimi na familia yangu tulikuwa mstuni kula chakula, unajua tena baridi sana hapa kwa hiyo watu muda mwingi wanakuwa ndani tu. Lakini leo jua na pia joto lilikuwa kidogo. nadhani mtajiuliza tulikula nini jibu ni kwamba tulichoma soseji na pia mikate

na yasinta


Hej på er alla läsare det är min första blogg. Idag jag och min family har varit i skugen och grillade korv.


av yasinta