NIMETUMIWA HUU UJUMBE NIMEONA NISIWE MCHOYO WA ELIMU:-
Nyoka uliyembeba kwenye mzigo wa kuni kutoka shambani anaweza kukuumia nyumbani wakati unatua mzigo. Siyo kila unayemsaidia lazima akusaidie, wengine inabidi wakuumize ili ujifunze. Kuna watu wanajifunza vizuri baada ya kuumizwa. Kwa hiyo katika maisha tunahitaji watu wote; wazuri na wabaya. Wazuri watakupa furaha, wabaya watakupa uzoefu ndiyo maana imeandikwa mpende adui yako, ila angalia asikuue, maana ukifa hutojifunza kitu!
Imeandikwa na Mwl. Denis Mpagaze.
Kkkkkk. Ni kweli. Kikulacho ki nguoni mwako dada. Habari za siku nyingi hata kama umenichunia wala sijui sababu.
ReplyDeleteNipo hewani na mm dada yangu tangu 2007 tulikuwa wote na kiss cha KOMBA na akinaKOMBA kombat mnyana na kombat binadamu
ReplyDeleteMIMI ISACK AU NAPENDA NIITWE che jiah
ReplyDeleteDa Yacinta habari za siku nyingi. Sisi huku tunalima summer tu na winter tunagandisha na kuendelea kuhomola. Tafadhali ondoa huo ujumbe juu wa utapeli na kutangaza upumbavu. Huyo aliyeweka ujumbe huo na kuficha ujumbe ni shetani binadamu anayetaka kuwaliza watu akidhani ni wapumbavu kama yeye. Tafadhali ondoa uchafu huu. Kwangu ukiwekwa nauporomosha siku hiyo hiyo maana kuna mipumbavu inayotaka kutumia blog za wenyewe kutanganza uchafu na utapeli wake. Ondoa tusitapike aghaaa aghaaa!
ReplyDelete