Monday, October 28, 2019

AINA MBALIMBALI YA VIFAA VINAVYOTENGENEZWA NA UDONGO WA MFINYANZI



Soko la vyungu vya asili vinavyotokana na udongo wa mfinyanzi. Si rahisi hasa kwa vijana wetu waliokulia mjini kufahamu umuhimu wa vyungu hivi. Kwani vijana wa zamani tunakumbuka jinsi mama zetu, shaangazi zetu na bibi wazaa mama au baba jinsi walivyotumia vyungu hivi kupikia na jinsi chakula kilichotoka humo kilivyokuwa na ladha na utamu wa aina yake. Lakini pi tunakumbuka jinsi ambavyo vyungu hivi vilitumika kama jokofu. Kwa kuweka chungu kilichojaa maji juu ya mafiga matatu, na kuweka mchanga chini ya chungu na kunyunyizia maji mchanga huo, maji yalikua yakipoa na kuwa ya baridi kana kwamba yametoka kwenye jokofu.

No comments:

Post a Comment