Friday, February 23, 2018

BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO YATIMIZA MIAKA KUMI LEO!!

Hapa ni mwenyewe dada/mama Maisha na Mafanikio Leo!!!

Mmmmhh! Miaka KUMI leo imefika kama mchezo!!!!
Blog ya Maisha na Mafanikio kama mchezo leo yatimiza miaka kumi (10) kamili. Napenda kuchukua nafasi hii na kusema:- Hii yote ni kutokana na uwepo wenu ulioambatana na upendo pia ushirikiano mzuri mlio nao. Na kubwa zaidi ni kwa familia yangu kwa kuwa bega kwa bega nami. Pia napenda kusema kwa kupitia michango ya wasomaji na wanablog wenzangu nimeweza kijifunza mambo mengi sana. Na ndiyo kwa sababa hii napenda kusema:- AHSANTENI SANA KWA USHIRIKIANO WENU NASEMA TENA KWANI NAAMINI BILA NINYI, NISINGEFIKA HAPA NILIPO LEO. KWA KWELI NAAMINI KUWA SISI SOTE NI NDUGU NA NI WATOTO WA BABA MMOJA. UPENDO NA UMOJA WETU UDUMU DAIMA NA PIA MILELE!!!!!......Halafu la kufurahisha siku niliyoanza kublog ilikuwa ni JUMAMOSI na leo ni IJUMAA... HAYA IJUMAA  IWE NJEMA SANA KWA WOTE MTAKAOPITA HAPA NA WENGINE WOTE.

5 comments:

  1. HONGERA SANA, KWA KAZI HIYO NZURI YA KUJALI WENGINE NA KUTOA KILE ULICHOJALWIA NACHO KWA AJILI YA WENGINE, TUZIDI KUWA PAMOJA, HONGERA KWA KAZI NZURI TWAKUOMBEA UZIDI KUWA NASI .

    ReplyDelete
  2. Ahsante sana sana tena sana. Narudia tena uwepo wenu ndio umenipa moyo

    ReplyDelete
  3. Hakika siku hazingandi lakini zinayeyuka kimyakimya.
    Hongera kwako na wadau wote wa kibarazani.

    ReplyDelete
  4. Yaani kakangu usemacho ni sahihi kabisa maana naona kama ni juzi nilianzisha hiki kibaraza chetu....Ahsante sana kwa uwepo wako na wengine wote wanaopita hapa waachao mchango na hata wapitao tu MBARIKIWE SANA.

    ReplyDelete