Thursday, June 22, 2017

MLO WA MCHANA WA LEO:- UGALI,TEMBELE NA DAGAA

 Kuna watu tembele wanaona kama mboga duni sana, wanakosa uhondo kwa kweli. Ni hivi:- kwanza chambua vizuri, kisha osha tembele lako, mimi huwa naanika kidogo lakini kuna wengine wanapika moja kwa moja baada ya kuosha yaani bila kuanika. Weka sufuria/chungu motoni, weka mafuta ya kutosha, maana tembele linahitaji mafuta la sivyo utalichukia na ndio sababu wengi hulalamika matembele sio mazuri, kumbe mapishi duni. Tia kitunguu geuza geuza kisha tia nyanya zako na chumvi kidogo. Nyanya zikiiva weka tembele lako. Ligeuze hapo mpaka linywee weka maji kidogo sana kisha funika, sio sasa ndo utoke....utaunguza. Watakiwa uwe hapo hapo unalichungulia kama limeiva. Ukiona bado ongeza maji kidogooo usiweke maji menge, ukiona linanywea zaidi hapo mambo tayari/limeiva.
Mwisho mwidho kamulia kipande cha ndimu au limau geuza dakika mbili -tatu  tayari kwa kula sasa.
UGALI,TEMBELE NIMEONGEZA NA DAGAA
Weka mezani kama hutakipenda hiki chakula, basi nimeshindwa. NATUMAINI UTAJILAMBA VIDOLE:-) MCHANA MWEMA.

4 comments:

  1. Nimekitamani chakula, mate yananitoka.
    Matembele yanaitwaje kwa kiingereza?

    ReplyDelete
  2. karibu sana usiye na jina...jaribu k-google kwani hata mimi sijui

    ReplyDelete
  3. Habari zenu, nipo hapa kushuhudia, jinsi nilivyo kuwa mwanamitindo tajiri na maarufu duniani mwenye mafanikio makubwa, nimekuwa nikipitia magumu miaka nenda rudi, tangu nilipofiwa na wazazi wangu wote wawili, sikuweza kuendelea zaidi na mshikaji wangu kutokana na Suluhu la kifedha basi, hadi miezi mitano iliyopita, nilimaanisha rafiki ambaye aliniingiza kwenye familia ya freemason, mwanzoni niliogopa kujiunga, kwa sababu nimesoma habari nyingi za uongo kwenye mtandao kuhusu familia ya freemasonry, na ambayo sasa ninaijua. hiyo sio kweli, zote zilikuwa habari za uongo, na napenda kutumia fursa hii kusema asante sana kwa familia ya freemason, ndugu wote wa familia hii, nawashukuru sana kwa support mnayonipa, na kwa waliodhani familia ya freemasonry ni mbaya, haijui sheria na kanuni za huyu jamaa, tafadhali acha kuhukumu ulikuwa hujui, na acha kusambaza habari za uongo, kama una nia ya kuwa mwanachama ufurahie. faida za familia ya freemasonry, contact off anuani icial hapa chini kwa taarifa zaidi.

    WhatsApp; +31 687 329 133
    Barua pepe; info.masonic.oregon@email.cz
    Barua pepe; info.masonic.oregon@gmail.com
    Au soma zaidi kuhusu sisi kwenye kiungo cha ukurasa wa Facebook; https://web.facebook.com/infomasonicoregon

    ReplyDelete