Hebu angalia huyo mama, yaani sasa badala ya kubeba mtoto mgongoni amebeba kuni na mtoto tumboni. Halafu huo mzigo wa kuni ni bonge la mzigo na ukiangalia kwa pembeni kabania na mboga majani ....Ila mimi nina swali kwa nini asingebeba hizo kuni kichawani ?Na hapo nadhani akifika nyumbani ni kwenda kuteka maji au kutwanga pia. Hakika hapa ndio pale tunapotakia kuwa na usawa....tujadili pamoja
Huyu mama hajawahi kuwa huru na anahitaji ukombozi wa kweli. Sijui kama mchango wake kwa taifa na dunia unathaminiwa. Inasikitisha sana tena sana tu.
ReplyDeleteHivi hii hali itakuwa hivi mpaka lini? maana mwanzo tulikuwa tukisema hatuna uhuru na sasa miaka zaidi ya hamsini lakini hali ile ile ...
ReplyDelete