Wednesday, September 7, 2016

NJIA NZURI YA KUWEZA KUTAFAKARI PALE UNAPOPUMZIKA NI KWENDA MSTUNI ...KAPULYA WENU HUTUMIA MUDA HUO KUTAFUTA UYOGA NA KUTAFAKARI....

Leo ni siku yagu ya mapumziko, na siku kama hii napendakuitumia kwa kwenda mstuni kutafuta uyoga. Ndiyo natafuta uyoga, lakini la muhimu zaidi kwangu ni  kunyoosha viungo na bila kusahau kuwa mstuni peke yako ingawa hujui kama upo peke yako ni njia moja ya kufikiri mambo mengine katika maisha. Ila pia  kama leo nimepata kitoweo:-)
JIFUNZE KUTAFAKARI KWA KWENDA MSTUNI:-)  KWANI NI SEHEMU TULIVU SANA...

4 comments:

  1. Bado Sweden mna misitu ya kwenda kuokoteza uyoga! Lucky you! Hata hivyo, habari za siku nyingi? Unapaswa kunyoosha viungo kabla winter haijaingia kuvikunja.

    ReplyDelete
  2. Misitu ni mingi sana ni nafasi yako tu....na kipindi hiki cha kipupwe uyoga ni mwingi sana...yaani umeifanya jioni yangu iwe ya kicheko eti napaswa kunyoosha viungo kabla winter/baridi haijaingiakuvikunja....kaaazi kwelikweli. ..oh za siku nyingi ni safi sijui huko wenzetu. ...

    ReplyDelete
  3. Za siku nyingi poa. Siku moja nitatia timu lau nami nichume huo uyoga nilete hapa nyumbani.

    ReplyDelete