Hapa sijui mapozi au ndo furaha
Baada ya kuangalia sana nikaona nywele zangu si nyeusi si isipokuwa zimepata ugeni ...angalia tu utaona :-) Unajua nini nimependa sana hiyo na naahidi sitamfukuza mgeni huyo kwani kuna wengine wanamtafuta ...Ila duh sijui nitaweza kuchana kila siku maana ni kipilipili/ulezi hasa
UMEKUWA MWAFRICA HALISI DADA
ReplyDeleteHujambo Yasinta binti Ngonyani?
ReplyDeleteEster mdogo wangu....ahsante.Ila ni mwafrika halisi tangia...nilijificha tu labda.
ReplyDeleteKaka Ray! Mie sijambo.
Hujambo da Yasinta? Umependeza kweli kweli. By Salumu.
ReplyDeleteKa'Salumu...kitambo hujaonekana mie sijambo. Ahsante kwa mtazamo wako...
ReplyDeleteMimi najua siku zote u mwafrika. Sema uko orijino kabisa. Je hiyo ving'aravyo ni mvi au macho yangu?
ReplyDeleteKwa ujumla umetokelezea na kupendeza dada.
Kaka Mhango! Ahsante. Macho yako yapo sahihi kabisa ni muvi. Ahsante tena-:)
ReplyDeleteHongera, ndugu yangu, ukiona hivyo ujue ule umri wa hekima zaidi umeingia. Enzi hizo wewe unapewa mamlaka na heshima kwenye vikao, lkn huku bongo, kwa hivi sasa ukianza kufikia huo umri unaanza kuogopa...ila nikuambie kitu, Utu uzima dawa. Tupo pamoja
ReplyDeleteemu thtree! Ahsante...Unajua ni juzi tu ilikutana na mdada mmoja akaniangalia sana kiasi kwamba nikajisikia aibu...nikashindwa kuvumilia kama nilivyo na ukapulya wangu nikamuuliza kulikoni....akasema una mvi lakini unaonekana u msichana mdogo sana ...nilicheka sana...Nawe ndugu yangu unasema ingekuwa enzi hizo ningepewa mamlaka na heshima kwenye vikao...Kaaazi kwelikweli...Pamoja daima.
ReplyDelete