Mwezi Machi, wakati wa msimu wa Kwaresima, shule zetu tatu za kitawa (
novisi) kutoka Benediktini ya jumuiya ya watawa ya Hanga, Mgimwa na Peramiho walikutana katika jumuiya ya watawa
Hanga kwa ajili ya semina ya wiki moja. Pia kulikuwa na novisi/watawa kutoka jimbo la Mtakatifu Paul iliyopo Lighano katika jimbo kuu la Songea. Mwalimu wa semina hiyo alikuwa
sista kutoka St Getrude Convent wa Imiliwaha katika Jimbo la
Njombe . Hakika, ilikuwa ni fursa kubwa kwa vijana hawa kuwa na muda
wa kuomba kwa
pamoja kijamii na chakula cha kiroho. Sisi sote tulipata
moyo kuona vijana hawa katika malezi, matumaini ya baadaye ya jamii zetu za kidini. Mungu awabariki!
No comments:
Post a Comment