MIAKA kadhaa iliyopita, “jumba [dogo] la makumbusho” lilianzishwa kwenye kituo cha kuteleza kwa ski cha Deux-Alpes, chini ya mlima wa Jandri Glacier, kusini-mashariki mwa Ufaransa. Sanamu moja ya barafu iliyoonyeshwa hapo ilikuwa sanamu ya mwuzaji wa vitabu na bidhaa. Sanamu hiyo ilikuwa ukumbusho wa biashara ya kale ya milimani ya wauzaji wa vitabu na bidhaa.
Kwa karne nyingi wauzaji hao wa vitabu na bidhaa walitembea kutoka soko hadi soko na nyumba kwa nyumba wakiuza bidhaa walizokuwa wakizibeba shingoni (jina la muuzaji wa vitabu katika Kifaransa ni colporteur, nalo linatokana na neno col linalomaanisha shingo, na porter linalomaanisha kubeba). Watu wengi leo hawajawahi kusikia juu yao. Na wale ambao wamekwisha sikia juu yao, huenda wakadhani kwamba walikuwa wachuuzi duni wa vitu visivyo na maana. Hata hivyo, wauzaji hao wa vitabu na bidhaa wangali na uvutano mkubwa katika maisha ya mamilioni ya watu hadi leo hii.
Nimeipenda taarifa hii. Nami hupenda kuweka taarifa za vitabu katika blogu yangu. Umenikumbusha mengi, kwani, ingawa natoka Litembo, Peramiho ni kama nyumbani. Kila ninapokuwa Peramiho, sherti niingie katika lile duka la vitabu. Ulienda tena hivi karibuni?
Ahsante kaka Ray kwa mchango wako. Prof:- Mbele...... vitabu ndio msingi wetu wa maisha... Kila niendapo nyumbani SIKOSI KUFIKA DUKA LA VITABU PERAMIHO kununua vitabu pia magazeti kama la Mwenge na Mlezi.. ndiyo nilikuwa karibuni huko:-)
Wauzaji wa Kale wa Vitabu na Bidhaa
ReplyDeleteNA MWANDISHI WA AMKENI! NCHINI UFARANSA
MIAKA kadhaa iliyopita, “jumba [dogo] la makumbusho” lilianzishwa kwenye kituo cha kuteleza kwa ski cha Deux-Alpes, chini ya mlima wa Jandri Glacier, kusini-mashariki mwa Ufaransa. Sanamu moja ya barafu iliyoonyeshwa hapo ilikuwa sanamu ya mwuzaji wa vitabu na bidhaa. Sanamu hiyo ilikuwa ukumbusho wa biashara ya kale ya milimani ya wauzaji wa vitabu na bidhaa.
Kwa karne nyingi wauzaji hao wa vitabu na bidhaa walitembea kutoka soko hadi soko na nyumba kwa nyumba wakiuza bidhaa walizokuwa wakizibeba shingoni (jina la muuzaji wa vitabu katika Kifaransa ni colporteur, nalo linatokana na neno col linalomaanisha shingo, na porter linalomaanisha kubeba). Watu wengi leo hawajawahi kusikia juu yao. Na wale ambao wamekwisha sikia juu yao, huenda wakadhani kwamba walikuwa wachuuzi duni wa vitu visivyo na maana. Hata hivyo, wauzaji hao wa vitabu na bidhaa wangali na uvutano mkubwa katika maisha ya mamilioni ya watu hadi leo hii.
(Chanzo:www.jw.org/sw)
Dada Yasinta
ReplyDeleteNimeipenda taarifa hii. Nami hupenda kuweka taarifa za vitabu katika blogu yangu. Umenikumbusha mengi, kwani, ingawa natoka Litembo, Peramiho ni kama nyumbani. Kila ninapokuwa Peramiho, sherti niingie katika lile duka la vitabu. Ulienda tena hivi karibuni?
Ahsante kaka Ray kwa mchango wako.
ReplyDeleteProf:- Mbele...... vitabu ndio msingi wetu wa maisha... Kila niendapo nyumbani SIKOSI KUFIKA DUKA LA VITABU PERAMIHO kununua vitabu pia magazeti kama la Mwenge na Mlezi.. ndiyo nilikuwa karibuni huko:-)