Nimeyatamani kweli machungwa...Niwaambie kitu nilipokuwa mwanafunzi wa darasa la kwanza na pili. Shuleni kwetu Lundo kulikuwa na miti mingi sana ya matunda mbalimbali mojawapo machungwa...Basi nakuambieni baada ya shule unaaga nyumbani kwenda kuchota maji au kuokota kuni kumbe kula machungwa ya shule...shhhh.:-(.....Ila mmhhh ilikuwa ukikamatwa na mlinzi basi ni viboko tu ...Kaaazi kwelikweli:-) PAMOJA DAIIMA NA MWANZO MWEMA WA MWISHO WA JUMA. PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA. Kapulya.
Machungwa yenyewe unayotamani mbona mabichi? Ukikumbuka zama hizo unatamani siku zigandishwe au kurejeshwa nyuma lau ufaidi kidogo halafu urejee kwenye maisha yako.
ReplyDeleteJamani machungwa mnafaidi peke yenu. Na mie kidogo! By Salumu.
ReplyDeleteKaka Mhango! Ndiyyo ni machungwa mabichi...lakini kumbuka kuna mengine yanakuwa ya kijani lakini yameiva na åia kuna wengine wanapenda mabichi...Yaani natamani sana siku zirudi nyuma tena:-)
ReplyDeleteKaka Salumu! wala sijakunyima wewe kula na macho:-)