Hivi AMANI duniani imekwenda wapi? Maana sasa watu wanauana, wanachinjana na vita ndiyo kila kukicha. Je ndiyo mwisho wa dunia au Upendo na Amani vimetutoka? Ukikumbumba hasa kwa Afrika jinsi wote tilivyokuwa wamoja, wote tulivyokuwa kitu kimoja....Hivi vyote vimekwenda wapi...Naomba tujadili pamoja maana palipo na wengi pana mengi. Kapulya.
Hayo unayoona ni mambo ya kawaida duniani sema kilichobadilika ni upashanaji na upataji habari wa kasi kwa sasa. Watu huzaliwa na kufa na ni jambo la kawaida. Hivyo usipate taabu dadangu. Kua uyaone.
ReplyDeleteDada Yasinta, wa-Afrika, sawa na watu wengine, walikuwa wanachapana vibaya, na wakati mwingine walitafuta suluhu. Wakati mwingine waliweza kupata suluhu, na wakati mwingine walishindwa, wakaendelea kuchapana.
ReplyDeleteMifano ya karne za karibuni ni jinsi Shaka na watu wake wa kabila la Zulu walivyowachapa watu wa makabila mengi, wengi wakatoroka na kuishia sehemu ambazo leo tunaziita Zimbabwe, Zambia, Malawi, na Tanzania.
Afrika Magharibi, watawala kama Sundiata na Samori Toure walikuwa wakiwachapa wengine. Kwetu, wa-Hehe walichapana na wengi, wakiwemo wa-Ngoni.
Sisi wa-Matengo hatukuwa na mbavu kama wa-Ngoni, kwa hivi ilikuwa
wa-Ngoni walipokuja kutuchapa,
sisi tulikuwa tunatimkia milimani kwenye mapango kujificha.