Saturday, April 25, 2015

KARIBU:- KUNA USHIBE!!

Naanza bila mpango, Kwa tenzi pia na tungo,
Niyafumbue mafumbo, Ugali na mbogamboga.
Wanadharau mapishi, Wanayabeza mapishi,
Mapishi ya Waswahili, Ugali na mbogamboga.
Umeyasifu matango, Mazuri sana kwa macho,
Huleta ngozi nyororo, Ugali na mbogamboga.
Na uyoga asilia, Kushiba bila ya kula,
Nashiba na kutazama, Ugali na mbogamboga.
Ugali huo wa sembe, Sembe nyeupe pepepe,
Na dona usiutupe,Ugali na mbogamboga.
CHANZO : KWA MJENGWABLOG

11 comments:

  1. Msosi baba kubwa. By Salumu.

    ReplyDelete
  2. Kwnaza napenda kwakaribisha Vimax na Meizing Botanical karibuni sana na ahsante kwa mchango wanu. Kaka Salum ni kwel:-)

    ReplyDelete
  3. Hao vimax na meizitang si wa kukaribisha. Ni blog za kishenzi zinazodandia kwa wengine kutangaza utumbo wao uwe makini ili siku moja wasijeiteka blog yako.

    ReplyDelete
  4. Hee! kumbe Ahsante kwa TAARIFA KAKA MHANGO

    ReplyDelete
  5. Dona,mchicha na samaki,usitaje!

    ReplyDelete
  6. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete