Tuesday, March 10, 2015
MWANAMKE UNATAKIWA KUJITAMBUA!
Leo au niseme wiki hii katika pita pita zangu nimekutana na hii mada kwa dada Adela Kavishe nikaona si mbaya isambae haya karibu uungane nami....
Kila mtu anaweza kuwa na majibu tofauti pale anapoulizwa uzuri wa mwanamke ni nini? kuna atakayesema uzuri wa mwanamke ni muonekano wake, yaani umbo lake zuri la kuvutia, sura yake, miguu nk, lakini pia yupo atakayesema uzuri wa mwanamke ni kuwa na tabia nzuri ama uzuri wa mwanamke ni kujituma na kufanya kazi kwa bidii.
Majibu yote yanaweza kuwa na mtazamo tofauti, lakini ukimfikiria mwanamke mzuri ni yule ambaye anajitambua na kufahamu umuhimu wake katika jamii, mwanamke mzuri ni zaidi ya urembo wa sura yake, ama muonekano wake kumbuka sura nzuri haiwezi kudumu milele, kwani kuna siku itachoka na kuzeeka, muonekano wa mwili na wenyewe hubadilika siku zinavyozidi kwenda hata kama ufanye nini lakini mabadiliko katika mwili ni sehemu ya maisha ya binadamu, ila mwanamke ambaye ni mzuri kutokana na tabia yake, yaani mzuri kutoka moyoni siku zote atabaki kuwa mzuri haijalishi mabadiliko ya muonekano wake.
Mwanamke mzuri ni mwanamke anayemjua Mungu na anaishi akiwa na hofu ya Mungu, vilevile ni mvumilivu, mpole, na anayejua kuishi na watu mbalimbali wanaomzunguka katika maisha yake. Mwanamke mzuri sikuzote anajikubali katika hali yoyote iwe ni katika shida au raha, siyo muongo ni mkweli katika maisha yake na wakati wote anasimamia ukweli bila kuwa na hofu. Mwanamke mzuri hatakiwi kuwa na hasira ijapokuwa ni kitu ambaocho kipo katika maisha yetu.
Inapotokea unajiona umekereka na una hasira sana ni vyema ukajua namna ya kuzuia hisia zako ili usikurupuke kuchukua maamuzi ambayo yataleta madhara katika maisha yako, kumbuka kutafakari kila jambo kabla ya kuchukua maamuzi, Katika maisha ya mahusiano unaambiwa mwanamke mzuri sikuzote huijenga familia yake, na vilevile mwanaume yeyote ambaye unamuona anamafanikio katika maisha yake basi ujue kuna mwanamke mzuri ambaye amechangia kuwepo maendeleo hayo.
Mwanamke mzuri akipenda basi atakupenda kutoka moyoni lakini mwanamke mwenye tabia mbaya akikupenda utaona matokeo yake kwani migogoro itakuwa haishi hususani kama akiwa amekupenda kwasababu ya mali zako siku zikiiisha hawezi kuvumilia ila mwanamke mzuri atakuvumilia katika shida na raha.
Mwanamke mzuri anamvutia mwanaume mzuri, ijapokuwa wakati mwingine mwanamke mzuri anaweza kukutana na mwanaume mwenye tabia mbaya, na akavumilia, ila inapofikia wakati mwanaume huyo akazidisha manyanyaso kwa mwanamke huyu basi inampelekea kukakata tamaa na mwisho kulivua pendo, ukipata mwanamke mzuri katika maisha yako usichezee bahati muheshimu sana, na maisha yenu yatakuwa na furaha milele.
Mwanamke mzuri sikuzote anatafutwa na mwanaume aliye mzuri, na siyo yeye anamtafuta mwanaume.Mwanamke mzuri sikuzote anawaza mambo mazuri, ikiwa ni pamoja na mafanikio katika maisha kwa njia ya kujituma na kuwa mbunifu huku akifanya kazi kwa bidii kufikia malengo yake, Mwanamke mzuri siyo mbinafsi, atawasaidia na kuwashauri wanaohitaji msaada kutoka kwake kulingana na uwezo alionao mwanamke mzuri ana huruma na anafurahia mafanikio ya wenzake.
Ili kuwa mwanamke mzuri unahitaji kujitambua na kuwa na hofu ya Mungu atakusaidia kukabiliana na changamoto mbalimbali ambazo unaweza kukutana nazo katika safari ya maisha. Unaambiwa hakuna binadamu aliyekamilika lakini hakuna linaloshindikana kwa Mungu hata pale tunapokosea tunapiga magoti nakuomba msamaha na Mungu anatusamehe mara saba sabini, kisha maisha yanaendelea jambo la msingi ni kutambua kosa na kuwa makini usirudie kosa.
katika maisha furaha ni jambo la msingi sana na ili kuwa mzuri sikuzote ni vyema ukaitafuta furaha kwa kuishi vizuri na watu wanaokuzunguka, usiwe mtu mwenye visasi, hasira,majungu, ubinafsi, chuki, choyo na mambo mengine kama hayo Mwanamke mzuri unatakiwa kuwa na upendo kwa watu wote.UJUMBE NA ADELA KAVISHE.... HAPPY WOMEN'S DAY
Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani huadhimishwa kila mwaka nchini tarehe nane mwezi wa tatu. Mwaka huu kitaifa yanafanyika mkoani Morogoro yakiwa na Kauli Mbiu “Uwezashaji Wanawake, Tekeleza Sasa.”
KILA LA KHERI!!
HAKIKA NI UJUMBE MZURI SANA!( Ili kuwa mwanamke mzuri unahitaji kujitambua na kuwa na hofu ya Mungu atakusaidia kukabiliana na changamoto mbalimbali ambazo unaweza kukutana nazo katika safari ya maisha. Unaambiwa hakuna binadamu aliyekamilika lakini hakuna linaloshindikana kwa Mungu hata pale tunapokosea tunapiga magoti nakuomba msamaha na Mungu anatusamehe mara saba sabini, kisha maisha yanaendelea jambo la msingi ni kutambua kosa na kuwa makini usirudie kosa. katika maisha furaha ni jambo la msingi sana na ili kuwa mzuri sikuzote ni vyema ukaitafuta furaha kwa kuishi vizuri na watu wanaokuzunguka, usiwe mtu mwenye visasi, hasira,majungu, ubinafsi, chuki, choyo na mambo mengine kama hayo Mwanamke mzuri unatakiwa kuwa na upendo kwa watu wote.)
ReplyDeletehii nimeipenda sana
ReplyDeleteNadhani hata mwanaume au tuseme binadamu wote ni kujitambua. Tukifanya hivyo hatutakuwa na manyang'au kama CCM madarakani wakiiba na kufuja watakavyo wakati umma ukiteketea.
ReplyDeleteMke ambaye ni mfano mzuri anajitahidi kuijenga familia yake. (Soma Methali 14:1.) Tofauti na mwanamke mpumbavu ambaye haheshimu mpango wa ukichwa, mwanamke mwenye hekima anaheshimu sana mpango huo. Badala ya kuonyesha mtazamo wa ulimwengu wa kutotii na kujitegemea, mwanamke mwenye hekima anajitiisha chini ya mume wake. (Efe. 2:2) Mke ambaye ni mpumbavu haogopi kusema mabaya kumhusu mume wake, lakini mwanamke mwenye hekima anajitahidi kuongeza heshima ambayo mume wake anapata kutoka kwa watoto wake na watu wengine. Mke kama huyo anajitahidi sana kutodharau ukichwa wa mume wake kwa kumsumbua-sumbua au kubishana naye. Pia, anajitahidi kutumia pesa vizuri. Inaelekea kwamba mwanamke mpumbavu anatumia vibaya pesa ambazo familia yake inapata kwa shida. Mwanamke anayemuunga mkono mume wake hayuko hivyo. Anashirikiana na mume wake katika mambo ya kifedha. Anafanya mambo kwa busara na kutumia pesa kwa uangalifu. Hamsukumi mume wake afanye kazi nyingine ya ziada.
ReplyDeleteKaka zangu nawashukuruni sana kwa mchango wenu ...nitarudi kusema mawili matatu ...
ReplyDeleteMwanamke khanga....Asili ya mama mstaarabu wa Kitanzania.
ReplyDeleteKaka Nicky hakika umenena khanga ni vasi asili la mwanamkea hasa wa kiafrika.
ReplyDelete👵👵👵 happy woman's day
ReplyDelete