Thursday, January 29, 2015

TUSISAHAU METHELI ZETU:

1. Njaa ni adui, hata mchawi yaua.
2. Haki ya nyani kuona fahari kwa mkia wake
3. Heri yao wazee kujifunga kwa mshipi tumboni.
4. Yu mcheshi machoni moyoni kuna mengine.
5. Binadamu ujikaze, Mungu atakusaidia.
6. Ee mtoto utakutana na watu katili.
7. Yakiteguka mapaja choo hutoka ovyo.
8. Mtoto wa simba sharti naye awe simba.
9. Yu ndugu machoni
10. Fuata maji yanakokwenda.
Methali hizi nimezipata katika kitabu cha SIASA HAPO KALE  ni methali katika hadithi za kingoni. Ambazo zimetafsiriwa kwa kiswahili. Na kwa kingoni nimeweka kwenye blog ya vangoni.blogspot.com.

6 comments:

  1. NILIPAMISS HUMU NDANI BALAAA....SASA NIMERUDI...NAAMINI MU WAZIMA

    ReplyDelete
  2. Mwamba ngoma huvuta ngozi kwake. By Salumu.

    ReplyDelete
  3. Ester! Nashukuru umerudi nami nilikumiss. Wazima wote na naamini mu wazima pia.

    Kaka Salumu! Nimeipenda hiyo:-)

    ReplyDelete
  4. jamani mie hizi methali zote kwangu ni ngeni kabisaaaa.

    ReplyDelete
  5. Mama Wane ....hivi ndivyo tunavyojifunza

    ReplyDelete
  6. Dada Yasinta nina mda mrefu sikuingia umu ndani Leo nimefurai kuona tena blog yetu ya maisha na mafanikio

    ReplyDelete