Sunday, October 19, 2014
SAMAHANI KWA TATIZO LILILOTOKEA KATIKA BLOG YETU YA MAISHA NA MAFANIKIO..ILA SASA NATUMAINI ITAKUWA SWALI...
Hodi, hodi! ndugu zanguni. Mwenzeni ipo ila tu semeni nilitekwa ...kwanza niliona tarehe 14/10 Dada Ester Ulaya /mama Alvin aliniambia dada kuna shida hapa Maisha na Mafanikio vipi? Nikashtuka halafu nikaangalia ni kweli lakini baadae tatizo likatoweka na nikaweza kublog kidogo. Sasa 16/10 nikatumiwa na ujumbe wa barua pepe na Pro. Mhango naye akawa anaiambia dada Yasinta vipi naona umeteka maana nimejaribu kuingia nimeshindwa fanya hima na utufungulie . Nikawa sasa najiuliza mwanadada mimi nitafanya nini hapa. Nimehangainga weeee bila mafanikio naamaka leo asubuhi nakutana na ujumbe mwingine toka kwa kaka yangu Salumu naye anasema vipi dada ?..Mmmhh hapa kajasho kakaanza kunitoka maana nilijua lile swala limetoka. Sasa hivyo nimerudi nyumbani na nimefungua hili kopo kwa woga ...nikamwomba msaada baba watoto naye kwa vile ni mtaalamu kidogo wa komputer inaonekana amefaulu kuutoa ule ujinga. Shukrani nyingi sana kwake. Ahsante...Tuwe makini kutoweka link ambazo hazina sababu. TUPO PAMOJA DAIMA. NAWASHUKURU SANA WOTE WALIOIONA SHIDA HII NA KUNIPA USHAURI MAPEMA.
Asante da Yasinta. Naona mambo yamekuwa bambam. By Salumu.
ReplyDeletekaka Salumu Ahsante sana kwa kuwa bega kwa bega nami. Maana umenipa moyo na hasa nimshukuru sana Mr. bila hivyo peke yangu nisingeweza:-(
ReplyDeleteTunakukaribisha tena duniani da Yasinta. Tengeza backup kuepuka huu uhuni na usaka tonge wa kijinga. Je una habari za pro Matondo? Maana naona ameadimika sana.
ReplyDeleteKaribu tena, Nilishangaa kidogo maana kila nikijaribu ku-access yalikuwa yanakuja "mashikoro mageni"
ReplyDeletekaka Mhango! ahsante sana nitafuata ushauri wako. Alo sina habari na pro Matondo labda tumtangaze maana kweli kaadimika mno.
ReplyDeleteKaka Nicky ...ahsante sana alo nashukuru shem wako kanisaidia kutoa yale "mashikoro mageni" :-)