Ni raha pale wote mnaposaidiana kazi sio kumwachia mmoja tu. Hapa akina mama na watoto wanamenya karanga ingawa wengine wanapeleka mdomoni lakini wamejumuika kuifanya kazi...inavyoonekana ni karanga kwa ajili ya mbegu au labda kuunga mboga....Raha sana kushirikiana.....
....na hapa vijana hawapo nyumba wanasaidia kazi za nyumbani hapa wanakoboa mahindi. Wananikumbusha enzi hizi tulivyokuwa tukikoboa mahindi au kutwanga mihogo na kaka zangu. Nani anasema kazi ya kutwanga au kukoboa ni ya akina dada/mama tu? Nimependa sana hii Je na wewe umependa?:-)
Inapendeza kwa kweliii...
ReplyDeleteKachiki! Ni kweli kabisa nimekumbuka sana enzi zileeeee......
ReplyDeleteHata mimi nimeipenda sana inanikumbusha mbali kwani nimezifanya sana kazi hizo
ReplyDelete