Thursday, April 17, 2014

LUGHA NA MISEMO YAKE....

Mara nyingi nimekuwa mtu wa kupenda misemo ya lugha mbalimbali...KAPULYA..na hapa chini ni baadhi ya misemo niliyonasa. KARIBU

1. Mara nyingi anayetaka  zaidi ni tajiri kuliko hata anavyofikiria mwenyewe.
2. Hatuwezi kufanya kitu kizuri kwa haraka, kwa vile hatujui uharaka huo unaweza ukachelewa
3. Ndoto zetu hutimizwa kama kuna nia ya kutimiza.
4. Kucheka /kicheko ni dawa isiyoleta madhara
5. Tunazaliwa kama nakala halisi lakini tunakufa kama nakala
6. Kama una haraka kila mara, unalazimika kutulia na kusubiri  mpaka pale moyo wako utakapokuambia nini kufanya.
7. Kwenye matunda kuna mti.
8. Unapo wapa wengine furaha, na ndipo furaha huongezeka kwako pia.
9. Mimi ni mimi, lakini mimi ni mmmoja tu. Siwezi kufanya kila kitu, lakini naweza kufanya kitu fulani.
10.Unaweza kuwaza mambo mengi, lakini fanya kitu kimoja  kimoja.
ALHAMIS KUU IWE NJEMA KWA WOTE!!!!!

2 comments:

  1. Da Yasinta, nimeipenda hiyo 9. Mimi ni mimi, lakini mimi ni mmmoja tu. Siwezi kufanya kila kitu, lakini naweza kufanya kitu fulani. By salumu.

    ReplyDelete
  2. Yaani kaka Salum kama vile ulikuwa pembeni mwangu nami pia nimeipenda sana hiyo. Pamoja Daima:-)

    ReplyDelete