Saturday, April 26, 2014

HAYA NI MAPISHI YA JIONI YA JUMAMOSI YA LEO.......KARIBUNI KUJUMUIKA NASI!!

 Maandalizi:- Muhogo, Kabichi/Kebichi, kiazi kitamu, nyanya, binzari, chumvi, limau, kitunguu saumu,  kitunguu cha kawaida, tui la nazi, nyanya kopo,  maharagwe, mchele na mafuta.
 Wali wa nazi, Kachumbali, Maharagwe yaliyoungwa kitunguu, nyanya moja, chumvi na kijiko kimoja cha chai cha binzari, Kabichi/Kabichi iliyoungwa kwa nyanya na kitunguu, na mihogo na viazi vitamu vilivyokaangwa (chips)
Na hapa ndivyo ilivyoonekana sahani ya Kapulya jioni hii  na cha kuteremshia si kingine tena bali ni maji. KARIBUNI SANA...MIJA UPO...NA WENGINE WOTEEEE....TWAWATAKIENI JUMAMOSI NJEMA SANA WOTE!

13 comments:

  1. Duhh...Njaa,Usimalize KADALA.Nanyi muwe na J'mosi njema.

    ReplyDelete
  2. KACHIKI! Usiwe na shaka kipo kingi tu utakula mpaka kusaza......ahsante kwa yote:-D

    ReplyDelete
  3. Yaani ni chakula cha afya (diet), sio ile yenye minyama ya mafuta mafuta yanayo ongeza cholesterol. Heko da Yasinta kwa msosi mzuri! By Salumu.

    ReplyDelete
  4. Kaka Salumu..usengwili...mpaka nimejisahau na kukushukuru kwa kingoni. Nakwambia jana kulikuwa hakuna nyama wala samaki........ahsante na karibu

    ReplyDelete
  5. Naona Dada jana uliamua kabisa, hongera kwa mapishi. Mie nauliza hiyo mihogo umenunua wapi? Na je ni mitamu au?

    ReplyDelete
  6. Ndugu yangu!..hakika jana nikawaweka samaki pembeni pia nyama..nikapika mlo huu..tena maharagwe ni ya kutoka kwetu Songea mihogo inapatiikana kwenye maduka ya vyakula viazi pia hata ndizi za kupiks

    ReplyDelete
  7. Asante kwa taarifa ya wapi pa kupata mihogo. Ila ina maana maharage uliyobeba hayajaisha? mana naona umeandika ni ya Songea.

    ReplyDelete
  8. Karibu sana ndugu yangu...ni kweli ya kunyumba/Songea ...nilibeba mengiii si kwa ajili yetu tu na marafiki pia majirani wakikutembelea

    ReplyDelete
  9. Yasinta uchokozi huo...Eeebanaee!!!!

    ReplyDelete
  10. Jamani Mija... Nimefanya nini sasa..LOL Najua umetamani kweli hapo ulipo:-)

    ReplyDelete
  11. Huo msosi wa nguvu. wanawake mnajua kuchanaganya mahanjumati. yaani hapo unaposogea tu mezani unaanza kushiba.Hongra maana bado unakumbuka vyakula vya nyumbani

    ReplyDelete
  12. Duh,,,,dada hapo ukishiba unanyoosha kabisa na miguu...full afyaaa

    ReplyDelete