Tuesday, April 22, 2014

HALI YA USAFIRI VIJIJINI:- HII HALI MPAKA LINI?

Nimekaa hapa nikiwaza jinsi enzi zileee nilipokuwa msichana mdogo. Shule moja, Kanisa moja, Hospital moja, gari moja la kijiji. Na hapo gari hilo lilikuwa likisafiri  kwa wiki mara moja, na  ujue likiondoka kurudi majaliwa. Hii picha haihusiani na maelezo yangu ila tu inafanana sana. Hasa nilipokuwa nikienda shule kutoka kijijini kwetu Kingoli na Litumbandyosi kwa kuchapa mwendo mpaka Peramiho kwa muda wa siku mbili.  Alan Ntimba kama unasoma hapa najua nawe unakumbuka sana safari zetu za kwenda shule. Alan Ntimba ni rafiki yangu tulimaliza shule ya msingi pamoja.  Kama kuna mtu anajua habari zake TAFADHALI  nijuze au wewe mwenyewe Alan. Tulikuwa tukipata gari ambaloi  limejaa kiasi hicho bahati sana. Juzi tu nilikuwa nikienda kumsalimia baba mkubwa Litumbandyosi usafiri ni bado  yaani barabara si  za kuridhisha. Je? hii itakuwa hivi mpaka lini? Au je ule Ujamaa bado upo? Maana naamini ilikuwa vile kwa vile tuliishi sana kijamaa....Mmmmm nawaza tu kwa sauti...
TUPO PAMOJA!

4 comments:

  1. Kwa kweli nchi yetu Tz inahitaji viongozi wasio na tama ili kuweza kuiendeleza nchi badala ya wao kujilimbikizia. Hayo ndio maisha halisi ya mtanzania anayeishi kijijini! Mungu iponye Tz na watu wake.

    ReplyDelete
  2. Hapo ni afadhali kunapitika, hujafika maeneo mengine, huko msimu wa mvua ndio basi tena, kutembea kwa miguu...yah, maisha bora hayo

    ReplyDelete
  3. Hayo ndo maisha ya watu wa dunia ya tatu kwa maeneo ya vijijini. Lkni pia kuna maeneo mengine ya mijini yana tabu hyohyo. Yani kuzaliwa nchi hz imekuwa kama nia ajali ya kijiografia
    By shem wako mshana

    ReplyDelete