Picha hii imenikumbusha enzi hizo:Amka, amka kumekucha x2 Twendeni shuleni. au Panda, panda panda, panda mlima panda panda.....hapo mtu ulishaoga na sasa josho linakuvuja tena ...Duh kaazi kwelikweli....Je? hapa ni mazingira ya wapi katika Tanzania yetu?
Hizi ndizo changamoto za kwetu.
ReplyDeleteKaka Ray! Kumbe ni kwenu/kwetu hapa...Nimefurahi kusikia:-)
ReplyDeletePicha hii inanikumbusha mbali sana. Hapo mkononi nilikuwa na dumu la maji au mzigo wa kuni au tita la nyasi. Mguuni hakuna kiatu, kaptula yangu ina vilaka kama viwili hivi, shati sina uhakika ni rangi gani. Nafika shuleni naambiwa nimechelewa namba. Nachapwa viboko kwa kuchelewa namba, viboko vinafumua vilaka vyangu na kunilazimu kwenda kushona upya. Hela ya kupeleka kwa fundi hakuna, naishia kushona kwa mkono. Mmmh!! Kama si Mungu aliyekuwa pamoja nasi, mwanadamu na aseme sasa.
ReplyDeleteMlongo wa nene kaka Mhagama! Yaani umenikumbusha pia halafu hapo sasa si viboko tu hapana unapewa na adhabu ya kumwagilia maua au kesho yake uje na mzigo wa kuni..mweee....kaaazi kwelikweli..Ama kweli Mungu alikuwa nasi.
ReplyDeleteduh...hii picha imenikumbusha kijijini kwetu nilikosoma
ReplyDeleteMama Alvin! unaona mambo ya kale yalivyo na kumbukumbu...Kale wanafunzi walikuwa makini sana kuliko sasa. Maana sasa mambo ni mengi mno .....
ReplyDeleteDah..Dada Yasinta hii picha imenikumbusha mbali sana hadi machozi yamenitoka.Jamani Tusisahau tulikotoka.
ReplyDeleteManka! Naamini ni machozi ya furaha yalokutoka.....ama kweli tusisahau kabisa tulikotoka.
ReplyDeletevimax thanks gan infonya vimax asli di tunggu info selanjutnya gan obat klg
ReplyDelete