Sunday, February 23, 2014

BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO YATIMIZA MIAKA SITA LEO!!!

Hapa ni mwenyewe dada/mama Maisha na Mafanikio Leo!!!

Mmmmhh! Miaka sita leo imefika kama mchezo!!!!
Blog ya Maisha na Mafanikio kama mchezo leo yatimiza miaka sita (6) kamili. Napenda kuchukua nafasi hii na kusema:- Hii yote ni kutokana na uwepo wenu ulioambatana na upendo pia ushirikiano mzuri mlio nao. Na kubwa zaidi ni kwa familia yangu kwa kuwa bega kwa bega nami. Pia napenda kusema kwa kupitia michango ya wasomaji na wanablog wenzangu nimeweza kijifunza mambo mengi sana. Na ndiyo kwa sababa hii napenda kusema:- AHSANTENI SANA KWA USHIRIKIANO WENU NASEMA TENA KWANI NAAMINI BILA NINYI, NISINGEFIKA HAPA NILIPO LEO. KWA KWELI NAAMINI KUWA SISI SOTE NI NDUGU NA NI WATOTO WA BABA MMOJA. UPENDO NA UMOJA WETU UDUMU DAIMA NA PIA MILELE!!!!!......Halafu la kufurahisha siku niliyoanza kublog ilikuwa ni JUMAMOSI na leo ni JUMAPILI.... HAYA JUMAPILI IWE NJEMA SANA KWA WOTE MTAKAOPITA HAPA NA WENGINE WOTE.

16 comments:

  1. Hongera sana Mungu akusaidie uzidi kusonga mbele mbele zaidi.

    ReplyDelete
  2. hongera sana. Ila nauliza hiyo skirt uliyovaa ni mtindo gani? Sijaielewa kabisa na ningependa kujua mana naona mshono wake umenichanganya. Siku njema.

    ReplyDelete
  3. Da Yasinta, heko kwa kutimiza blogu yako miaka sita. nakumbuka kulikuwa na "Counter" ya kila nchi wanaotembeleya blogu yako, imeenda wapi? By Salumu.

    ReplyDelete
  4. Hongera Maisha na Mafanikio kwani juhudi na mchango wako tunauona na kuufaidi. Unasalimiwa na kaka yako Freethinking.
    Mungu akuongezee umri na maarifa uendelee kufaa na kupambana katika dunia hii ya ushindani.

    ReplyDelete
  5. Hongera sana Dada Yasinta.Siku njema

    ReplyDelete
  6. Hongera sana KADALA,MUNGU azidi kukufunulia na kukulinda kila iitwapo Leo..
    Pamoja Sana.

    wako KACHIKI.

    ReplyDelete
  7. Hongera Sana Da yasinta na Ubarikiwe..

    ReplyDelete
  8. HONGERA SAAAAAN DADA YANGU.....BLOG YETU IDUMU ZAIDI NA ZAIDI

    ReplyDelete
  9. Hongera sana jirani ..Najua sio kazi ndogo.Kila jema ktk maisha..Binafsi karibuni nitarejea

    ReplyDelete
  10. Nachukua nafasi hii na kuwashukuru wote kwa kuwa nami kusherehekea miaka hii sita ya blog yetu ya Maisha na Mafanikio. Kama nilivyosema bila ninyi ndugu zangu Maisha na Mafanikio isingetimiza miaka sita leo. Michango yenu ni changomoto kubwa sana kwangu...Inamfanya mtu awe na moyo wa kuendelea kuwa hewani. AHSANTENI SANA...PAMOJA DAIMA...KAPULYA:-)

    ReplyDelete
  11. Hongera sana Maisha na mafanikio kwa kutimiza mwaka mwingine. Kwa kupitia blog hii tumejifunza mengi, na kuburudika pia.

    Twakuombea wewe mpendwa wetu, Yasinta, akuzidishie afya nje,baraka na mafanikio njema uzidi kutupa zaidi.

    ReplyDelete
  12. Hongera sana Maisha na mafanikio kwa kutimiza mwaka mwingine. Kwa kupitia blog hii tumejifunza mengi, na kuburudika pia.

    Twakuombea wewe mpendwa wetu, Yasinta, akuzidishie afya nje,baraka na mafanikio njema uzidi kutupa zaidi.

    ReplyDelete
  13. Bora kuchelewa kuliko kukosa kabisa (sijakwambia nilikua nauguza pia)
    Hongera sana rafiki yangu kwa kuendesha uwanja huu ambao umetusaidia na kutunufaisha wengi.
    Mimi binafsi kutokana na baraza hili nimepata faida ya kuwa na Rafiki wa hiari! (Iko siku naomba uweke makala maalumu nipate kuwaelezea wenzetu hapa urafiki wetu ulipoanzia na wewe umekua ni mtu wa namna gani katika maisha yangu)
    Kwa leo niishie kwa kusema Hongera sana, tunakuombea kwa Mungu maisha na afya njema, na baraza letu lidumu!

    ReplyDelete
  14. emu-three! Ahsante sana kwa yote.
    Rafiki yangu wa hiari!..Wala hujachelewa tupo pamoja..Nitakutafuta

    ReplyDelete
  15. Hongera sana mtani kwa kufikisha miaka sita ya kublog. Ama hakika katika kipindi hiki umetujuza mengi mno yenye kuelimisha, kuburudisha na kufikirisha bongo zetu kwa kiwango kikubwa. Ninajisikia raha sana kuwa familia ya wanablog.

    Kila la kheri. Daima mbele.

    ReplyDelete
  16. Mtani wa mimi! Ahsante sana...ni furaha liioje kusoma maoni yako. Tupo pamoja daima.

    ReplyDelete