Saturday, January 18, 2014

HAYA NI MAPISHI YA KAPULYA JIONI HII YA LEO..KITIMOTO NDANI YA UYOGA......

 Ni kitimoto, uyoga niliochuma mwezi wa kumi, cream kidogo, nyanya , chumvi na maji kidogo na viungo vingine....
 Na baada ya muda chakula kilikuwa tayari kuliwa na hapa ni shani yangu, ikiwa imeshehena na wali, kitimoto,uyoga  kama hapo juu na sallad tamuuuu ambayo ni:- nyanya, tango, carroti, majani ya salladi na chizi(fetaost) na kitunguu kwa mbaliiii...
Nikapandishia na glasi ya maji kama uonavyo...Ila usisite kuja kuna chakula bado karibu sana tena sana kujumuika nasi. JIONI NJEMA.

8 comments:

  1. Wewe! Haramu hiyo. Usitake kugombana na watu. Mie hiyo kitu huwa haipandi japo sizuiliwi na imani yoyote zaidi ya kumuona mnyama mwenyewe kama hana adabu vile na ana mifuta kibao.
    Uyoga na kitimoto wapi na wapi da Yacinta. Muhimu usinikaribishe. Kula mwenyewe unenepe kama kitimoto mwenyewe.

    ReplyDelete
  2. Mwal. Mhango...nimecheka kweli jioni hii...ila najua ungeonja nilivyopika ungependa ni filet hakuna mafuta hata kdidogo.....ila naheshimu msimamo wako ...lakini huko na hii baridi ingewafaa:-D

    ReplyDelete
  3. Safi sana da yasi we mkali Pia maeneo hayo.huyo asiyekula unamkaribisha bila kumwambia ni kitimoto.akijilamba mwisho ndo unamwambia kanguruwe kenyewe kalikua kadoogo wala hakajanona sana mwee.akajinyonge mbele

    ReplyDelete
  4. Kaka Isaac wewe...mkali pia ngoja siku yako tufanye sherehe ya kitimoto ba tuwaalike wote bila kuwaambia ni kitoweo gani...Lolo

    ReplyDelete
  5. Wow! We onja on my behalf hiyo kiti moto hata uiite majina ya kitasha bado ni kitimoto. Enjoy ila mifuta ikipanda usilalamike. Kweli hii kitu inaweza kuwa yum. Acha niishie usniweke majaribuni bure.

    ReplyDelete
  6. Mwal.Mhango..Yaani hakuna siku nimecheka kama leo ...baada ya kusoma maoni yako:-) mifuta ipo katika vyakula vingi na katika hii ni hiari yako kuamua kula na mifuta au kutoa. Pia si kitimoto tu mtu unaweza kupanda hata vyakula vingine pia kama vile mikate nk...Haaaa haaaa kukutia majaribuni eti?? kumbe umetamani eeehhh...LOL

    ReplyDelete
  7. Nistamani unadhani hilo pishi nchezo dada yangu. Acha hii kitu ipigwe marufuku na kuwa haramu ingwa siyo. Vitamu vingi vina mambo yake.

    ReplyDelete
  8. Ahsante mwl. Kk Mhango..kwa kupenda pishi langu....mmmmh kupiga marufuku watawakomoa wengi...

    ReplyDelete