Mmmmmhhh!! Mwenzenu nimeka hapa nikiwa na mawazo kibao ....maisha haya hakika nimekumbuka mno ...UGALI WA MUHOGO na samaki halafu ukiongezea na matembele au kisamvu....basi tu . Sasa leo kisa cha kukumbuka hili ni kwamba ninajiuliza nipike nini maana nilitaka kupika ugali lakini sasa UNGA sina na kama mnakumbuka nililima bustani na niliweka akiba sasa unga sina nipo hoi hapa. Mboga ipo ila sina unga. Basi mawazo yakaja na kukumbuka wakati nilipokuwa KADALA kama huyo binti kutwanga na kuchekecha na mwisho mtu unakuwa unga tu mwili mzima...JE KUNA ANAYEKUMBUKA KAMA KAPULYA HAPA?
Yani umetukumbusha mbali sana! ugali ugali ugaaaaaaaaaliiiiii hamu ya ugali kwa mboga za majani. Sasa Yasinta ina maana unga ulioleta toka Tz umeisha mara hii???????Jamani uwe unabeba mwiiiingiiiiiii saaaaaaaaana sana halafu unalipia ile uzito unaozidi ili nasie tuukute haujaisha, ona sasa unga umeisha hata sijafika kwako kula ugali jamani jamani. Haya ukanunue wa njano wa Sweden ujichane ila hauna hata ladha!
ReplyDeleteUsiye na jina!..yaani hakuna chaula kitamu kama ugali na mboga za majani. Ndiyo unga niliobeba umaniishia sikubeba mwingi na unajua sasa na hizi mboga nikawa najipikia tu kila siku kwenda kuangalia mama weeee umeisha..ila kuna unga fulani si wa njano nitautafuta huwa nanunua.....mazoea hujenga tabia kwa kweli
ReplyDeleteUgaliiiiiiiiiiiiiiii,ugaliiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii ndiyo maisha na mafanikio yetu.
ReplyDeleteKaka Ray! Yaani haswaaa bila ugali hakuna maisha na mafanikio...Lol
ReplyDeletevimax thanks gan infonya vimax asli di tunggu info selanjutnya gan obat klg
ReplyDelete