Hicho chungu cha bluu ndio mmea wa dodoki/madodoki mwenyewe umekuwa na umetambaa mpaka kwenye paa ya varanda...sasa leo nimegundua -----
Mmea huo umeanza kutoa maua na pia dodoki zimeanza kujitokeza hakika nimefurahi sana. Ila sasa najiuliza nitaumewka wapi maana kaubaridi kameanza na mmea huu unataka joto ....maana mwisho wako
...ndo dodoki linakuwa hivi hapa tayari lishakomaa na kukauka tayari kwa kujisugulia mwilini. Hili nilinunu Songea Sokoni mwaka huu...Kweli hili hapo juu karibu na ua litakuwa kama hili?...Mwenye ushauri naomba tafadhali!! Nawatakieni jioni yenye upendo na amani.
Uhamishe sitting room isije ikapata snow na kujifia. Vipi mapapai bado? By Salumu.
ReplyDeleteKaka Salumu! Nikihamishia sitting room basi itabidi mwenyewe nisikae hapo maana linatambaa kwa haraka kweli ....Ahsante kwa ushauri
ReplyDeletelabda uliingize ndani likae karibu na dirisha liwe linapata mwanga
ReplyDeleteMhhh;sawasawa kabisa!
ReplyDeletedodoki in english wanaitaje
ReplyDeleteRidge gourd i think so..
Delete