Wednesday, September 4, 2013

LEO TUANGALIA JIOGRAFI,HISTORIA YA MJI WETU WA SONGEA!!!

Leo tuangalia mji wa SONGEA:-
Songea ni mji nchini Tanzania ambao ni makao makuu ya Mkoa wa Ruvuma. Kulingana na sensa ya mwaka 2002 idadi ya wakazi wake ilihesabika kuwa 131,336. Kuna barabara ya lami kutoka Songea kupitia Njombe hadi barabara kuu ya Dar es Salaam - Mbeya. Barabara ya kwenda pwani kupitia Tunduru na Masasi ni mbaya mara nyingi haipitiki wakati wa vua haswa..ila sasa iko mbioni kutengenezwa...
JIOGRAFIA KIDOGO:-
Mji wa Songea uko kimo cha M 1210 juu ya UB katika nchi ya Ungoni kwenye nyanda za juu za kaskazini za Tanzania. Chanzo cha mtu Ruvuma kipo karibu na mji.
HISTORIA:-
Jina Songea ni kumbukumbu ya chifu Songea wa Wangoni aliyekuwa na ikulu yake hapo wakati wa kuenea kwa wa ukoloni wa Ujerumani akauwawa na Wajerumani wakati wa vita ya majimaji.
Mji wa Songea (iliandikwa Ssongea wakati ule) ulianzishwa mwaka 1897 kama kituo cha kijeshi cha Kijerumani. Ukakua kuwa makao makuu ya utawala wa mkoa wa Songea wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani.
Mazinginra ya mji yaliathiriwa vibaya na vita ya majimaji na ukandamizaji wake na Wajerumani.
Songea ikaendelea kuwa makao makuu ya mkoa wakati wa utawala wa Uingereza katika Tanganyika na baada ya uhuru katika Tanzania huria.....HII NI HISTORIA/GEOGRAFIA YA MJI WA SONGEA...

5 comments:

  1. Mhh, tunashukuru sana kwa darasa hili kumbe Songea inatokana na jina la kiongozi wao, mimi nilichukulia matamshi yake, nikahisi linatokana na neno `sogea'...mmh, kama ilivyo neno wangoni, nikachukulia kuwa linatokana na neno `UGONI...' kUMBE SIVYO,shukurani mpendwa

    ReplyDelete
  2. emu-three! umenifanya nitabasamu kidogo hapa ,,,yaani tafsiri yako.

    ReplyDelete
  3. Asante kwa historia mji wa Songea dada Yasinta na karibuni Moshi mjini.
    ===================================

    Moshi ni makao makuu ya Mkoa wa Kilimanjaro nchini Tanzania.
    Wakazi
    Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2002, mji huu una wakazi wapatao 144,739 [1]. Kabila linaloongoza kwa idadi ya wakazi wa mji wa Moshi ni Wachagga wakifuatiwa na wapare na makabila mengine yaliyohamia kutoka sehemu mbalimbali za tanzania kama wasambaa,warangi n.k. Wachagga wanapenda vyakula vinavyopikwa kwa kutumia ndizi kama vile mtori, kitawa, na machalari.
    Wakazi wengi wa Moshi ni wakulima, wafugaji na wafanyabiashara. Watu wengi wanaenda mjini Moshi kufanya kazi na kurudi nyumbani jioni.
    Ukuaji wa mji wa Moshi hauendani na mipango halisi ya 'Mipango Miji'. Hii inatokana na kutokufuatiliwa kwa sheria mbalimbali zinazohusu uendelezaji wa miji.
    Hali ya Hewa
    Moshi ni mji wenye baridi katika miezi ya Juni mpaka Agosti na kipindi cha joto katika miezi ya Oktoba hadi katikati ya Januari.
    Utalii
    Mji wa Moshi una mandhari nzuri ya kuvutia watalii. Watalii hupenda sana mji wa Moshi kwa sababu ya mlima Kilimanjaro na huduma muhimu kama mahoteli na usafiri.
    Elimu
    Mji wa Moshi una vyuo vikuu vitatu:
    • MUCCoBS (Moshi University College Of Cooperative and Business Studies) ambacho ni chuo kikuu kishiriki cha Sokoine University of Agriculture (SUA) Morogoro
    • MWUCE (Mwenge University College Of Education) ambacho ni chuo kikuu kishiriki cha SAUT (St. Augustine University - Mwanza)
    • KCMC Medical School chini ya Chuo Kikuu cha Tumaini
    • O.U.T(The Open University of Tanzania) ambacho ni tawi la chuo chenye jina hilohilo chenye makao yake makuu jijini Dar es salaam.--
    Utawala
    Kiutawala mji wa Moshi ni wilaya ya Mkoa wa Kilimanjaro. Ndani yake kuna kata 15 ambazo ni Bondeni, Kaloleni, Karanga, Kiboroloni, Kiusa, Korongoni, Longuo, Majengo, Mawenzi, Mji Mpya, Msaranga, Njoro, Pasua, Rau, Mfumuni na Kilimanjaro

    ReplyDelete
  4. Sina haja ya kuharibu mada kwa kuleta historia ya mji wangu. Kimsingi da Yacinta umeniacha hoi ulipotumia analogue ya NCHI YA UNGONI. Du! Nchi ndani ya nchi! Kweli Tanzania ni jamhuri ya Muungano. Hata hivyo, somo zuri sana. Emu-Three taratibu. Una maana Kigoma inatokana na mgomo au tuseme Mbeya ni wambeya ukiachia mbali Kibondo kupenda bondo na Ntwara twala.

    ReplyDelete
  5. Na safari ijayo tutaendelea na somo letu la kujua Miji/nchi nadani ya Nchi...Ahsante wote

    ReplyDelete