Friday, September 27, 2013

LEO NAPENDA NIWAPELEKE MPAKA NYUMBANI KWETU LITUMBAND´YOSI ..HAPA NI SHULE YA MSINGI AMBAYO MDADA MIMI NIMEWAHI KUSOMA ...

SHULE YA MSINGI LITUMBAND´YOSI
Leo nimekumbuka sana nyumbani yaani kule alikozaliwa baba yangu ndiko kwa mimi ni nyumbani kwangu....Nikakumbuka shuleni  hapa jinsi tulivyokuwa tukikutana shule nne kwa mashindano ya Kililupa..ikiwa na mana shule ya msingi Kingoli, Litumband´yosi,  Luhagara na Paradiso. Ilikuwa ni michezo ya kata. Najua wengi mliosoma shule hizi nayi mtakumbuka jinsi ilivyokuwa....Nawatakieni wote Mwanzo mwema wa mwisho wa wiki

14 comments:

  1. Duh!! Hii kiboko. Nilikuwa najaribu kuvuta kumbukumbu huu ni upande gani. Nimekumbuka shule inaonekana hivi ukiwa upande wa barabarani pale kwenye miembe mingi(sijui kama bado ipo).
    Nilisoma hapa hadi nilipomaliza darasa la tatu ndipo nilipohama na kwenda kuendelea na darasa la nne katika shule ya Msingi Mapinduzi (Peramiho).
    Naikumbuka KILILUPA kuliko unavyoweza kufikiri. Wakati nikiwa darasa la pili nilishiriki kwenye kikosi cha MGANDA. Mashindano yalifanyika Kingoli na kikosi chetu kilichukua ushindi wa pili katika mganda. Mengine sikumbuki yalikuwaje zaidi ya huo mganda wangu. Darasa la tatu mashindano yalifanyika Luhagara. Nilisusa kwenda dakika za mwisho baada ya Mwalimu wa mganda (Mzee Sambalitola) kunitukana tukiwa kwenye riheso. Wakati wa kuondoka nikatoroka, ameenda kushtuka katikati ya safari kwamba sipo kwenye msafara wa kwenda Luhagara.
    A wonderful Flash Back.

    ReplyDelete
  2. Ni mpenzi wa lugha ya nyumbani na ana kipaji kujua lugha za wengine, najua ni wachache wanamudu hilo... lakini ameweza kujifunza lugha za wanyasa wale wanaongea kama wamalawi.... kimatengo... kingoni chenyewe, kimanda, kimpoto.... kinyakyusa..... nk. Ukitaka kufikia maisha na mafanikio ni lazima uupende na kuutambua utamaduni wako na kuuheshimu ule wa wengine .
    Hana majivunao na hupenda kubadilishana mawazo na watu mbali mbali, na pia hupenda kufuatilia habari za nyumbani kwao alikotoka na haoni haya kuongea lugha ya kwao ya kingoni chenye ladha ya kimanda na kuhanikizwa na ghani ya kindendeule.
    Daima hujitambulisha kwa jina la asili ya kwao na huona fahari kutumia jina hilo.
    Makazi yake ya sasa ni ughaibuni katika ardhi ya waswidi na hajafunga milango kwa uzao wake kutambua na kuenzi asili ya mama yao ijapokuwa wao ni wazawa wa ughaibuni, amekuwa msitari wa mbele katika malezi ya wanae ili kuhakikisha wanae hao hawajitengi na asili ya aliotoka yeye.

    ReplyDelete
  3. Kaka Njau, wewe ni mwandishi wa mashairi?

    ReplyDelete
  4. Mlongo wa nene kaka Mhagama...Hata mimi leo nimekumbuka mengi mengi sana na mimi nilikuwa na michezo mitatu kwaya, Netboli na kukimbia basi wewe kazi kweli. Halafu nilichokuwa napenda zaidi pale mnapokuwa katika shule ya ugenini basi wanafunzi wenyeji wanakuwa ndio wenyeji wenu yaani mnachukuliwa na kwenda kwao na mwisho unakuwa urafiki au undugu...Nimejenga urafiki na undugu kwa njia hii.

    Kaka Ray! nami nauliza kama kaka Mhagama hivi ww ni mshairi maana duh! nusu nilie hapa:-)

    ReplyDelete
  5. Yasinta Ngonyani ni mpenzi wa lugha ya nyumbani na ana kipaji kujua lugha za wengine, najua ni wachache wanamudu hilo... lakini ameweza kujifunza lugha za wanyasa wale wanaongea kama wamalawi.... kimatengo... kingoni chenyewe, kimanda, kimpoto.... kinyakyusa..... nk. Ukitaka kufikia maisha na mafanikio ni lazima uupende na kuutambua utamaduni wako na kuuheshimu ule wa wengine .
    Hana majivunao na hupenda kubadilishana mawazo na watu mbali mbali, na pia hupenda kufuatilia habari za nyumbani kwao alikotoka na haoni haya kuongea lugha ya kwao ya kingoni chenye ladha ya kimanda na kuhanikizwa na ghani ya kindendeule.
    Daima hujitambulisha kwa jina la asili {Yasinta Ngonyani} ya kwao na huona fahari kutumia jina hilo.
    Makazi yake ya sasa ni ughaibuni katika ardhi ya waswidi na hajafunga milango kwa uzao wake kutambua na kuenzi asili ya mama yao{Lundo-Nyasa} ijapokuwa wao ni wazawa wa ughaibuni, amekuwa msitari wa mbele katika malezi ya wanae ili kuhakikisha wanae hao hawajitengi na asili ya aliotoka yeye.( Mimi Ray Njau siyo mshairi bali ni mdau na mtetezi wa lugha ya Kiswahili)

    ReplyDelete
  6. Nimeipenda hiyo habari aliyoandika Kaka Ray njau, jamani Yasinta ni dada anayestahili sifa zote hizo. jamani she is sooooooooooooo niceeeeeeee, nampendaje dada Yasinta sasa! Kwa kweli huwa nikiongea naye kwenye simu sitaki hata kumaliza. Kwa kweli mume wako na watoto pia wana raha sana kuwa na mama kama wewe. Yasinta tupe siri ya maisha yako, au ni malezi uliyoyapata tangu utotoni. Mungu akubariki dada Yasinta.

    ReplyDelete
  7. Ni kweli Enzi michezo mashuleni ilikuwa burudani na sehemu ya kujenga umoja n upendo baina ya vizazi
    hali hiyo ikirudi tunaweza kurejea katika mfumo wa jamii iliyokuwa una utaratibu wa kujenga maadili na utii kwa ujumla.
    Kila la kheri Tanzania Nema na yenye upendo na amani.
    Wajenzi wa Tanzania yenye neema na amani ya kweli na utii ni mimi na wewe.
    Kila la kheri na hongera kwa kukumbuka ulikotoka na kulikulea!

    ReplyDelete
  8. Ahsante kaka Ray...Na usiye na jina wala sina siri yoyote zaidi ya malezi niliyoyapata na pia zaidi kuwa mimi.
    Kaka Salehe Nyumbani ni nyumbani hata kuwa vipi...na kweli siku zile mashuleni kulikuwa na barudani nyingi na wanafunzi walikuwa wakakamavu.

    ReplyDelete
  9. Kaka Mhagama umeniwahi, lakini acha nami niulize tu,,

    Hivi kaka Ray Njau wewe ni mshairi?

    Kwako dada mkuu Yasinta.."Kila siku nakwambiaga wewe ni kiboko"

    God bless.

    ReplyDelete
  10. Kwangu ushairi zero,japo kwa kunusa najaribu.Mapenzi kwa Kiswahili,utetezi ndiyo nguzo.Asante na salamu Mija wewe pokea.

    ReplyDelete
  11. Kaka Ray pengine unahitaji kuwezeshwa ili uweze kuwa mshairi. Maana hata majibu yako yamekaa kimashairi mashairi. Na kwa kuwa una mapenzi makubwa na lugha ya Kiswahili, basi ushairi ungekuwa msaada mkubwa kwako katika kutimiza lengo.
    Jaribu, unaweza.

    ReplyDelete
  12. Shukrani zangu ndiyo asante wewe Imanueli hapa nakutaja.Kaya ya Mhagama wewe kwako chimbukoni.Uwepo wako hapa thamani usoni pangu,madokezo yako hakika najali na kujaribu maishani nguzo yake mafanikio.Kibaraza kiwepo daima,makutano yetu kituoni.

    ReplyDelete
  13. vimax thanks gan infonya vimax asli di tunggu info selanjutnya gan obat klg

    ReplyDelete