Nimekumbuka nikiwa nimeshaanza kukaanga kuwaonyesha tangu mwanzo..ni hivi unahitaji unga wa ngano, chumvi kidogo, sukari kidogo, mafuta na maji moto hivi nifanyavyo mimi .Unakanda unga na hivyo nilivyotaja na baadaye unasukuna na hapa chapati ikiwa kwenye flampeni inakaangwa
Na hapa tayari zipo zinasubiri walaji, chapati, kuna chai ya rangi na ya maziwa na wale wanaotumia sukari ipo kwenye hichi kibweta cheusi kwa hiyo karibuni sana tujumuuke.JUMATATU NJEMA KWA WOTE.
Ukarimu wako ni wenye thamani sana japo kwa macho kuona; nami nasema asante sana!
ReplyDeleteKweli kabisa nilidhani ni yai kabla sijasoma maelezo...
ReplyDeleteZinaonekana tamu ile mbaya.
Hongera kwa kipaji cha kupika.
Kaka Ray! Chakula kinanoga mkiwa wengi.....karibu sana.
ReplyDeleteDada mkuu msaidizi! ni tamu sana wahi basi ujumuike nasi...tena kimbia
kwa! huku sasa ni kuringishiana! sasa huku madongo kuinama nitakaribiaje chapati huko kwenu? Haya mi nimebaki ka mzee fisi...kudos my sis zinaonekana ni tamu kweli!
ReplyDeleteJamani chapati zinakwisha! Msinisahau na miye! By Salumu.
ReplyDeleteYasinta leo asubuhi ni chapatti,kwa kweli nimezitamani sana ila ndio hivyo siwezi kuwahi. Ila siku nikija ntaomba na chapatti uniandalie.
ReplyDeleteKaka Mrope! Eeeeh kwanza karibu tena maana ulipotea kiduchu. Et madongo kuinama nimecheka:-D kweli hapa. Usikond utazikuta zipo nyingiiii.
ReplyDeleteKakangu Salumu! Haziishi na wala hujasauliwa.
Usiye na jina! Wala usikonde utapata tu. Nakusubiri kwsa hamu na mlango upo wazi
Da yasinta zinatamanisha kweli, mmmh,
ReplyDeleteDa yasinta zinatamanisha kweli, mmmh,
ReplyDeleteKaribu Nancy karibu sanatujuike di unajua chakula mkiwa wengi kinavyonoga.
ReplyDelete