Friday, August 9, 2013

IJUMAA YA LEO :-KUMBUKUMBU KITABU CHA JUMA NA ROZA

Nakuambia kitabu hiki nimekisoma na nilikuwa nakipenda sana..hadithi hi imekaa kichwani utafikiri sala la baba yetu au wimbo wa Taifa...Je Unaikumbuka pia?

7 comments:

  1. Halafu iili tusisahau tukawa tunapocheza ule mchezo wa kuruka kamba basi tukawa tunaimva hivi :- ELiza, beee, watoka wapi? Natoka shule...kufanya nini? Kusoma kitabu..
    Kitabu gani? Cha Juma na Roza.......iikuwa raha kweli

    ReplyDelete
  2. Dar Yacinta umenirudisha nyuma kama miaka 40 hivi. Shukrani sana kwa kutuletea historia ya safari yetu kitaaluma.

    ReplyDelete
  3. Dah, mimi sijawahi soma hiyo hadithi. Dada Yasinta nimependa namna unavyokumbuka mambo ya kitambo uliyowahi kuyapitia. Hii inadhihirisha jinsi ulivyo makini na mambo unayosoma. SAFI SANA DADA YANGU!

    ReplyDelete
  4. Habari.
    Hicho kitab umenikumbusha jinsi tulivyokuwa tunakariri kusoma kupitia kwa mwalimu,ikitokea unaambiwa onyesha mstari kwa
    Mstari ilikua inakua taabu.
    Lakini vilikuwa vinavutia na kufanya mwanafunzi atake kujua kusoma. Umesahau kumtaja Damasi na Mwanasesere.
    Nadhani pia unakumbuka hadithi zilizoko,Bulicheka na Lizabeth na melikebu, Mpiga filimbi wa melini.
    Kila la kheri.

    ReplyDelete
  5. Ahh, hicho kitabu kimenikumbusha mbali.
    Na hivyo ndio vilikuwa vitabu vya kuanza kufunua aili za watoto wetu, si upupu wa siku hizi.



    ReplyDelete
  6. Jamani naomba mwenye nakala ya kitabu hiki aniuzie nimfundishie mwanangu, kilikuwa kitabu mtambuka kwa sie tuliojaaliwa kukisoma, aliyetoa copy ya jarada lazima atakuwa nacho, madukano havipo tena. justin@juasun.net

    ReplyDelete