Friday, June 28, 2013

NIWATAKIENI IJUMAA HII YA MWISHO WA MWEZI KWA MLO HUU...MAKANDE!!!

Karibuni tujumuike na mlo huu wa makande/ngánde/makandi..au sijui wewe kwa lugha yako unasemaje..Nimeona si vibaya kama Ijumaa hii ya mwisho wa mwezi huu tukimaliza kwa mlo huu mzito.Ijumaa njema na mwisho wa juma uwe mwema kwa wote.

17 comments:

  1. Usangi hiyo naiona mbele yangu, kishukuri chedi.

    ReplyDelete
  2. Watani zangu wapare shughuli imempata mwenyewe au???????????

    ReplyDelete
  3. emu-three!! nafurahi kama nimekufikisha kunyumba.
    Nancy!..kwanza karibu sana kibarani..na ahsante
    Kaka Ray..:-)kumbe ni chakula muhimu cha wapare? mimi nilikuwa najua hasa kule ubenani na upangwani...

    ReplyDelete
  4. Dada yani hapo nipo nyumbani yani umenitamanisha sana

    ReplyDelete
  5. Amina....karibu ...au je huwezi kuandaa unajua vyakula vingine huwa tunasahau tupo na ugali kila siku..

    ReplyDelete
  6. Watani zangu wapare hizo ni pure ja spesheli avae!

    ReplyDelete
  7. Ahsate dada yote haya nikujiendekeza tunasahau vakula vaasili eti mpaka uende nyumbani ndio ule tena kwa mwaka mara moja ngoja nianze kudumisha mila

    ReplyDelete
  8. Kaka Ray...hiyo lugha imenishinda wapare labda wanisaidie
    Amina! Ni kweli lazima kudumisha mila nipo tayari kuwa pamoja nawe.

    ReplyDelete
  9. Pure ja spesheli avae, me mwnyw mpare ila hapo cjamsoma vyema, unajua dada ngoja nkwambie kitu yaani wapare tupo magroup mng kweli nahis hicho kipare ni cha same na nlichosema mm (kishukuri chedi)yaani makande mazuri hicho ni cha usangi dadaangi dadaangu.

    ReplyDelete
  10. Safi sana wanikumbuka mbeya Milima ya Uporoto kabisa. Nimesahau email yako nataka nikutumie habari fulani unitafsirie


    ReplyDelete
  11. Nancy! nimekuelewa na kama umekaribia basi nasema tena karibu sana.
    Kaka Nicky! nafurahi kama umepata kumbukumbu ya milima ya Uporoto..Kuhusu email jaribu kuangalia tena utaipata
    Ahsante kaka Ray..naona wote Nancy na mimi na wengine tumepeta jibu.

    ReplyDelete