Monday, June 24, 2013

NIMERUDI KUJA KUANGALIA BUSTANI YANGU MARA MOJA...HIVI NDIVYO BUSTANI ILIVYO BAADA YA MWEZI MMOJA...MTOTO WA MKULIMA NI MKULIMA!!

 HAPA NI MBOGA YA MABOGA ..TENA ILE YA NJOMBE(NYAMUZA) AU PITIKI/SUKUMA WIKI..IMEKUWA HIVI BAADA YA MWEZI MMOJA
 NYANYA ZIMEANZA KUTOA MAUA
 SALLADI AINA YA RUCCULA
 STRAWBERRY/STROBERI
 AINA YA VIUNGO/ÖRTKRYDDOR
 VIAZI MVIRINGO
 VITUNGUU
 FIGIRI
Na hapa ni matokeo ya mboga ya maboga mnayaona mchuma wa kwanza. Kwa hiyo leo ni chakula kila nikipendacho ugali, mboga na maharaga hivi hapa maharage yapo jikoni. Mchicha bado kidogo haujakua ..nitawaonyesha ukikua...Si mnakumbuka hapa....... KARIBUNI TUJUMUIKE KATIKA MLO HUU WA MIKONO YA KAPULYA WENU:-)JUMATATU NJEMA SANA KWA WOTE

15 comments:

  1. Mke mwenye uwezo, ni nani anayeweza kumpata?Thamani yake inapita sana ile ya marijani.Moyo wa mume wake umemtegemea, wala hakuna faida inayokosekana.Amemthawabisha mume wake kwa mema, wala si kwa mabaya, siku zote za maisha yake.Ametafuta sufu na kitani, naye hufanya kazi yoyote inayopendeza mikono yake.Amekuwa kama meli za mfanyabiashara.Huleta chakula chake kutoka mbali.Tena huamka kabla usiku haujaisha,na kuwapa watu wa nyumbani mwake chakula na kuwapa vijana wake wa kike fungu lao lililoamriwa.Amefikiria shamba, akalinunua;amepanda shamba la mizabibu kutokana na matunda ya mikono yake.Amejifunga nguvu viunoni, naye ameitia nguvu mikono yake. Ametambua kwamba biashara yake ni nzuri; taa yake haizimiki usiku.Amenyoosha mikono yake kushika kijiti cha kusokotea uzi, nayo mikono yake mwenyewe imeshika gurudumu la kusokota nyuzi.Amewanyooshea mkono wenye kuteseka, na mikono yake amemkunjulia maskini.Hana wasiwasi juu ya watu wa nyumbani mwake kwa sababu ya theluji, kwa maana watu wote wa nyumbani mwake wamevaa mavazi mawili.Amejitengenezea matandiko yenye mapambo.Mavazi yake ni ya kitani na sufu iliyotiwa rangi ya zambarau.Mume wake ni mtu anayejulikana malangoni,anapoketi pamoja na wanaume wazee wa nchi.Hata ametengeneza mavazi ya ndani na kuyauza, nao wafanya-biashara amewapa mishipi.Nguvu na fahari ndiyo mavazi yake, naye anaucheka wakati ujao.Hufungua kinywa chake kwa hekima,na sheria ya fadhili zenye upendo ziko katika ulimi wake.Anaangalia shughuli za nyumba yake, wala hali mkate wa uvivu.Wanawe wamesimama na kumtangaza kuwa mwenye furaha,mume wake husimama, naye humsifu.Kuna binti wengi ambao wameonyesha uwezo, lakini wewe—wewe umewapita hao wote.Uvutio unaweza kudanganya, nayo sura yenye kupendeza inaweza kuwa ubatili;lakini mwanamke anayemwogopa Yehova ndiye anayejiletea sifa.Mpeni baadhi ya matunda ya mikono yake, nazo kazi zake na zimsifu malangoni._Methali 31:10-31

    ReplyDelete
  2. Hongera kwa hatua ya kuchuma na kula sasa. Mie hicho chakula cha leo ugali, maboga na maharage nimevitamani, sasa sijui nitawahi hapo kwako au ntakuta umefunga na umeisharudi summerhouse? mana ni masaa kadhaa mpaka kufika huko! Au nipande ndege duh! Nachanganyikiwa sasa. Kwa kweli this time lazima nije kula vyakula vya shambani kwako. Au sijui unipostie mana nipo Sweden. Anwani yangu niliishakutumiaga dada.

    ReplyDelete
  3. Kaka Ray! ahsante kwa neno..pia ni somo la leo. Ubarikiwe sana.
    Usiye na jina!..wala usikonde nitakuwekea utakikuta tu hiki chakula na wala usichanganyikiwe ila wewe ndo unanichanganya mimi kwa kusema ulishanitumiaaga annwani yako...Hakina nina hamu kweli ya kujua wewe ni nani???

    ReplyDelete
  4. Dada Yasinta hongera kwa kazi nzuri unayoifanya, kweli wewe ni mtu mwenye bidii sana kimaendeleo. Nakutakia mafanikio zaidi katika maisha yako! By Salumu.

    ReplyDelete
  5. Dada Yasinta umenitamanisha sana na hiyo mboga ya maboga ,ningekuwa karibu ningekuja kula ugali.nikija kwenda home na mie nitajitahidi nikumbuke mbegu.Bustani imestawi hongera sana.kweli mtoto wa mkulima ni mkulima.

    ReplyDelete
  6. Kaka Salumu! Ahsante kwa kunitia moyo. Karibu ujimuoke nasi.

    Manka! Pole kwa kukutamanisha..kwani upo mbali sana ungekuja tule na mbegu ungepata maana hapa aloba haiozi.

    ReplyDelete
  7. Yasinta ni mfano wa kuigwa, haya kwa wale wanaoishi majuu, ambao hamjishughulishi na shughuli za kilimo wakati hali ya hewa inapokuwa nzuri kwa kulima tujifunze kwa dada yetu Yasinta. Mana watu kuja ulaya wanadhania ndio kutupa kila kitu kuja kula vyakula vya wazungu mwanzo wa mwaka mpaka mwisho haipendezi. Yasinta ni mfano wa kuigwa kwa wote watakaosoma mesg. hii tubadilike hasa kama una uwezo huo na eneo kaeneo ka kulima unako.

    ReplyDelete
  8. Kweli mtoto wa mkulima ni wa mkulima. Hongera sana MMC.

    ReplyDelete
  9. Usiye na jina! Sina budi kusema ahsante.

    Dada mkuu msaidizi (aka) Mija ahsante...na kumbuka mtoto umleavyo ndivyo akuavyo

    ReplyDelete
  10. hongera dada naona unajua kuriendesha riguwaride!! Hiyo yataka bidii ya hali juu hasa huko Ulaya. Mungu azidi kukiubariki wewe na familia..

    ReplyDelete
  11. Dada Yasinta nipo mbali itabidi tuongee vizuri dada yangu unitumie hizo mbegu za maboga na mchicha ha ha haa..kwenye bustani yangu hivyo ndivyo vilivyokosekana

    ReplyDelete
  12. Kaka Mrope! unajua vitu vingine kama hizi mboga mboga inabidi kujishughulisha hata kama huna eneo kuna aina ya makopo unaweza kupenda..Ahsante kaka nawe salamia familia..Na karibuni kula

    Manka! hamna shida nipo na hakuna shida mbegu utapata tu ndugu wangu..nakusubiri:-)

    ReplyDelete
  13. kwani una eneo kubwa kulima hzi mboga? upo safi sana nakupenda

    ReplyDelete
  14. Hongera sana KADALA..MUNGU azidi kukubariki na kubariki kazi za mikono yako!!!!!!

    ReplyDelete
  15. Hongera sana Da' Yasi (a.k.a Kapulya). Mboga zinanipa uchu kama nini kwa kuziangalia tu pichani. Endeleza libeneke la kuandaa!

    ReplyDelete