Kugega mdala= Kuoa mke
Kama wote tujuavyo:- Kijana na msichana wakikua, wanaoa. Kwa wangoni, mtoto wa kuime hata kama akikua na kuoa atakuwa bado anahitajika kwenda vitani. Kipindi hicho yupo vitani inabidi aonyeshe nguvu zake zote. Kijana ambaye hajaenda vitani huitwa "lijaha". Kijana aliyerudi toka vitani huitwa "lidoda". Mwanamkewa kuolewa inabidi awe wa uhakika, anayeweza kufanya kazi za nyumbani. Inabidi aweze kutafuta kuni, kuchota maji, kutwanga kupika ugali/chakula, kupika pombe na awe mchangamfu/mcheshi achekaye na watu wote mtaani/kijijini.
Ndoa haifungwi ndani ya ukoo. Kwa wangoni hairuhusiwi ni mwiko kuoa/kuolewa na mke/mume ambaye ana jina moja la ukoo. kama watu wakioana kiukoo, wazee wataulizia kwanza kama ukoo huo ni wa karibu au wa mbali? (vitepulana) wataapishwa. Watu wanaogopa kuoana ndani ya ukoo kwa vile watoto watakaozaa watakufa wote au watapata kifafa au hata waliokufa (mahoka) watakasirika. Watu wenye Kifafa na wenye ukoma ni mwiko kuoana.
MTENGA
Kwa kingoni cha zamani neno mtenga lilifahamika kama mtu aanyenunua au kuuza vitu. Pia Mtenga ni mtu auzaye mtoto wa kike. Yeye ndiye anayetoa mahali ya mwanzo na mahali yote kwa ukoo wa msichana.
VIPI KUTAFUTA MKE:-
Wenye mtoto wa kiume watakapo kumwoza kijana wao, wazazi wengine wanamtafutia mke, Wazazi wengine wanamwacha kijana wao ajitafutie mke ampendaye. Kama wame/watamwona msichana mzuri watatafuta mtu/ndugu ambaye watamtaka na watamwelekeza nini wanataka. Na huyo anaweza akawa MTENGA wao. Mtenga huyo ataanza kuulizia kisirisiri mambo ya wazazi wa msichana yule na ukoo wake wote na halafu ataenda kuwaeleza wazazi wa mtoto wa kuime. kama wazzi wakiona ya kuwa ni msichan huyu atamfaa kijana wao kama mke ,watenga wataenda kwa wazazi wa msichana tena na kutoa taarifa ya posa. Kama wenye binti watakataa, watenga/mtenga itabidi awabembeleze.....Itaendelea
Mila na desturi zetu ni muhimu sana, nyingine zilikuwa an hekima, ndio maana wazee wetu waliishi na kudumu kwenye ndoa zao
ReplyDeleteje umeamua kubadili muonekano wa rangi ya blog yako? wapi rangi ya pink? naona nyeupe kama sioni kitu vile!!bado nashangaa shangaa.
ReplyDeleteHATA MIMI NASHANGAAA HAPA NIMEKUWA SIJAINGIA TANGU JANA....NGOJA NITAFANYA UTAFITI..
ReplyDeleteNimeona dada... labda jamaa wa blogger wanazifanyia templates ukarabati. Natumaini mambo yatatengemaa...
ReplyDeleteKaka Mrope natumai kesho itakuwa kama kawaidi mara kila ninkiingia hapa naona kama nimepotea vile...
ReplyDeleteHaaaaaaaaaaaaa,haaaa;haaaaaaaaaa;ha,ha;ha;haaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!Huu ndiyo ujasiri wa jasiri asiyeacha asili ili asiwe hasidi na asiye na akili!!!!!!!!!
ReplyDeleteUmejitahidi sana. Tena sana nimefurahia sana kuona hivi
ReplyDeleteKaka Ray! Ahsante.
ReplyDeleteMarkus! Ahsante ndugu yangu...nami nafurahi kama umefirahi..unajua kstika msisha usisahau mizizo yako.