Saturday, June 29, 2013

KAMA WOTE TUJUAVYO AKIBA HAIOZI KWA HIYO LEO NI SIKU YA MAVUNO YA FIGIRI NA MBOGA MABOGA ..AKIBA

 Hapa Kapulya yupo kwenye bustani yake na hapo anachuma mboga ya maboga. Nimestuka ni vizuri kuweka akiba  maana msimu wa joto ni mfupi sana na muda si mrefu kutakuwa na baridi na sasa nitaweka akiba. Kuna aina mbili za kuweka akiba hizi mboga mboga na uyoga hata nyama na samaki...Kwanza unaweza kukausha kwenye jua au kuchemsha na kuhifadhi kwenye friza/jokofu na mimi nita...
chemsha  kama dakika 5-10 hivi na kuweka kwenye mifuko ya plastiki na kuweka kwenye friza  na nitakuwa nakula pale nitakapotamani..najua haiwi tamu kama kuchuma tu na kula..Hapa ni fungu moja la mboga maboga na fungu moja la figiri..mboga maboga ni mvuno wa pili na figiri mvuno wa kwanza...Kuhusu bustani....nitaendelea kuwajuza. Kwa hivyo usione unakosa  kuna akiba...karibuni na JUMAMOSI NJEMA ...TUONANE TENA PANAPO MAJALIWA....KAPULYA.

6 comments:

  1. aisee dada ntapataje mboga japo kidogo?next time nialike nikusaidie kulima

    ReplyDelete
  2. Kaka Ray! itakuwaje tena ikiwa hivyo?

    Kaka Isack! wewe njoo uchukue kuna nyingi tu yaani karibu..Wala usiwe na mashaka nitakualika unisaidie. Karibu!!

    ReplyDelete
  3. Da hongera sana dada umenipa changamoto nami ntakuwa mkulima bora, mpk natamani ningekuwa karibu nami nipate hapo mboga kdg. Hongera sana

    ReplyDelete
  4. Da hongera sana dada umenipa changamoto nami ntakuwa mkulima bora, mpk natamani ningekuwa karibu nami nipate hapo mboga kdg. Hongera sana

    ReplyDelete